Katika dakika zote tisini za mchezo, UDBS walionekana kuutawala mpira na kupelekea amsha amsha za hapa na pale katika lango la CASS.
Juhudi za CASS Kulinda lango lao lisiweze kutikiswa na UDBS zilishindwa mapema mwanzoni mwa kipindi cha kwanza ambapo UDBS walifanikiwa kujipatia goli safi na kuamsha hisia za ushindi.
Dakika 45 za kipindi cha pili ziliwatosha UDBS na wala sio CASS kupachika bao la pili. Bao hili lilifungwa na mshambuliaji machachali wa UDBS ( Carlic ) na kufunga ukurasa wa mabao katika mechi hiyo
Konahabari ilifanikiwa kurekodi jumla ya magoli mawili kwa UDBS na kushindwa kuandika chochote kwa CASS mpaka dakika ya 90. Michuano hiyo inaendelea katika uwanja wa mabibo ambapo timu nyingine zinaendelea kurusha karata zao.
Kikosi cha CASS kilicho fungwa bao 2 na UDBS.
No comments:
Post a Comment