Thursday, March 22, 2012
Wednesday, March 21, 2012
NAFASI ZA KAZI
AREA SALES MANAGER - 2 POSTS
Qualification: Degree in Marketing ,Business Administration,Economics or any other related field
Apply:Human Resources
Coca- Cola Kwanza
Box 2332, Mbeya
Details:The Guardian
March 14, 2012
Deadline: March 23, 2012
Qualification: Degree in Marketing ,Business Administration,Economics or any other related field
Apply:Human Resources
Coca- Cola Kwanza
Box 2332, Mbeya
Details:The Guardian
March 14, 2012
Deadline: March 23, 2012
Monday, March 19, 2012
AGOMBEA UBUNGE ALISHE FAMILIA.
Harakati za uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la Arumeru
mashariki zimekuwa zikichukua taswira tofauti ambapo CCM imeonekana kupata
ushindani mkubwa kutoka chama cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA ).
Akiongea na wananchi wa Arumeru
mashariki Mbunge wa Mtera ( CCM ),
Livingstone Lusinde aliwaomba wananchi wa jimboi hilo kumpigia kura
mgombea wa chama chake Bwana SIOI SUMARI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa
jimbo hilo ( Jeremiah Sumari ).
Lusinde aliitoa kauli hiyo katika
kampeni za kumdadi mgombea huyo zilizofanyika katika kijiji cha Migadini, kata
ya Mororoni ambapo kiongozi huyo alitoa
sababu mbalimbali za wananchi kumchagua mgombea huyo.
Lusinde alisema, wananchi
wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua mgombea huyo kwa kura nyingi
ili ajipatie mshahara utakao muwezesha kumudu familia aliyoiacha marehemu Baba
yake.
Mbunge huyo wa Mtera alienda mbali
zaidi kwa kusema “mkimchagua SIOI mtapata Baraka nyingi kwa Mungu kwa kuwa
mtakuwa mmemfuta machozi ya kufiwa na Baba yake, pia mtakuwa mmemfurahisha Rais
kwa kuwa SIOI ndiye chaguo lake.
Saturday, March 17, 2012
Marketing forum na mtazamo wa Vijana kujiajiri.
ukumbi wa Nkurumah wa chuo kikuu Dar es salaam
Wanafunzi na Wageni wakiandikisha ili kuingia katika ukumbi wa Nkurumah siku ya Marketing Forum 17/03/2012
IKUCHUKWU akitoa somo
Mahojiano ndani ya Nkurumah
Mwakilishi wa Azania Bank
Erick Tafisa akihojiwa na waandishi wa habari
Saa ya Chakula siku ya marketing forum
IKUCHUKWU akijibu maswali ya Vijana, full story
Dar es salaam University Marketing Association ( DUMA )
imefanya kongamano kubwa na waandishi wa habari, makampuni, taasisi za kiraia
na wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali nchini. Kongamano hilo limefanyika katika
Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es
saalam.
Maada kuu katika kongamano hilo ni nafasi ya Vijana
kujiajiri, ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa ziuzikazo katika masoko na
uendelezaji wa taaluma za wasomi ili kuyafikia mafanikio ya kweli.
Watoa
maada wakuu katika kongamano hilo ni
pamoja na IKUCHUKWU KALU- Mtaalamu wa masoko ya ndani na nje ya nchi na IMANI
KAJULA – Director wa masoko Benki ya NMB.
Kongamano
hilo limeanza saa tatu asubuhi ambapo Viongozi,wanachama wa DUMA na wageni
kutoka maeneo mbalimbali walikusanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu
Dar es salaam huku wakiwa na shauku kubwa ya
kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo masoko na fulsa zilizopo katika soko
la ajira.
Mwenyekiti
wa DUMA, Mr. Frank Minazi ambaye ni Mwanafunzi wa kitivo cha Biashara idara ya
masoko Chuo kikuu Dar es salaam alifungua kongamano kwa kuwakaribisha wageni
waalikwa na wote waliohudhulia. Baada ya utambulisho wa kiitifaki, mwenyekiti
alimkaribisha IMANI KAJULA kutoa maada kwa mamia ya watu waliokuwapo Nkurumah.
KAJULA
akiutumia vizuri uzoefu wake katika masoko alifanikiwa kuyaweka bayana mambo ya
msingi katika kuyafikia malengo, ikiwa ni pamoja na kujiamini kujituma katika
kazi, ubunifu na uwajibikaji. Hakusita pia kuelezea umuhimu wa makampuni,
taasisi na watu kujijengea imani na jamii wateja wao. Neno hili aliliita (
BRANDING ). Kwa mujibu wa Kajula, mtu anaye kuwa na sifa nzuri katika jamii,
Taswira ( image ) yake ni rasilimali.
IKECHUKWU
KALU, kwa upande wake alijikita zaidi kuelezea nafasi ya Vijana kujiajiri. Mtoa
maada alianza kwa kukili kuwa “ Ipo nafasi ya Vijana kujiajiri” mtazamo thabiti
( VISION ) na malengo ya muda mrefu ni
silaha muhimu katika kujiajiri, “alisema KALU”. Endapo vijana watakuwa na
mawazo thabiti inayoambatana na utekelezaji, basi wapo kwenye nafasi nzuri ya
kutengeneza ajira kupitia uvumbuzi.
KALU
alitoa mifano ya vijana wenye umri mdogo katika nchi zilizo endelea ambao
walifanikiwa kuanzisha makampuni makubwa duniani ambayo kwa sasa yanaajiri
idadi kubwa ya watu. Katika hili, hakuwasahau wagunduzi wa Facebook na Mozilla.
Vijana
waliuliza maswali mengi juu ya upatikanaji wa mitaji ili kujiajiri, hata hivyo
( KALU ) alisisitiza umuhimu wa kuwa na
mawazo thabiti” – VISION inayotekelezeka
kama msingi wa kujiajiri. Aliendelea kueza kuwa mafanikio madogo huandaa mazingira
mazuri ya mafanikio makubwa hivyo akasisitiza umuhimu wa matumizi mazuri ya
rasilimali kidogo tulizonazo katika kuandaa mazingira ya uwekezaji.
Kongamano
limeahilishwa, yapata saa kumi jioni………….
Kongamano hili kimedhaminiwa na TBC1, CLOUDS MEDIA, CREATIVE
EYE, NMB, CRDB, MLIMANI TV AND AZANIA BANK.
Imeandaliwa
na kuletwa kwenu na Konahabari.blogspot.com
Thursday, March 15, 2012
MKAPA AMKANA NYERERE ARUMERU
Akizindua kampeni za CCM kwenye uwanja wa michezo wa Ngaresero, Usa River Jumatatu wiki hii, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alisema:
“Nimefanya
kazi na Mwalimu kwa miaka 25, nikiwa mwandishi wake, Waziri na katika
muda huo, nimemzika yeye, kaka yake na mama yake mzazi, sijawahi kusikia
jina la Vicent Nyerere kama miongoni mwa wanafamilia ya Mwl. Nyerere.
Vicent ambaye ni mbunge wa Musoma mjini kupitia Chama Cha Demorasia ( CHADEMA ) alisikitishwa sana na kauli ya Mkapa na kusema si jambo la ajabu Mkapa kumkana yeye ( VICENT NYERERE ) kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao.
Mbunge huyo machachali wa Chadema amemtuhumu mkapa kuwa, akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.
Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi .
Vicent alimtaka Mkapa kuacha kujiingiza katika masuala ya familia yao baada ya MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere
Kwa sasa Vicent Nyerere anaendelea na kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki ambako Chadema kupitia mgombea wake Joshua Nasari anaonekana kuungwa mkono na wananchi wengi.
Mbunge huyo machachali wa Chadema amemtuhumu mkapa kuwa, akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.
Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi .
Vicent alimtaka Mkapa kuacha kujiingiza katika masuala ya familia yao baada ya MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere
Kwa sasa Vicent Nyerere anaendelea na kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki ambako Chadema kupitia mgombea wake Joshua Nasari anaonekana kuungwa mkono na wananchi wengi.
Monday, March 12, 2012
KONAHABARI: WANAFUNZI UDSM WAIENZI BAGAMOYO
KONAHABARI: WANAFUNZI UDSM WAIENZI BAGAMOYO: kulia ni katibu mkuu wa Accounting Association of Dar es salaam University ( AADU ) 2012, Mr Dayanus Mgaya akiwasubiri viongozi wa makum...
WANAFUNZI UDSM WAIENZI BAGAMOYO
kulia ni katibu mkuu wa Accounting Association of Dar es salaam University ( AADU ) 2012, Mr Dayanus Mgaya akiwasubiri viongozi wa makumbusho ya Bagamoyo.
Sahani hiyo inaonesha vifaa mbalimbali vilivyotumika enzi ya Utumwa zikiwemo fedha na shanga. Waarabu walijenga makazi yao katika eneo hilo ambalo linajulikana kama kaole. Neno Kaole limetokana na neno la "Chite chikalole Pumbuji" yaani twende tukaone wageni (waarabu).
Hapo juu ni wanafunzi wa kitivo cha biashara (B.COM) Chuo kikuu Dar es salaam wakiangalia picha za ukutani zinazoonesha maajabu mbalimbali ya Bagamoyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Accounting Association of Dar es salaam University, Bahati Steven akipongezana na katibu wa chama Mr. D. Mgaya.
Sanamu inayoonesha mateso makali waliyopata mababu zetu kwa kubebeshwa pembe za ndovu
Juu ni kisima cha maajabu kinachopatikana Bagamoyo, maji ya kisima hiki hayapungui wala kuongezeka katika misumu yote ya mwaka.
Wanafunzi wakinawa maji yanayotoka katikka kisima kisichokauka. inasadikika kuwa maji haya yanabaraka za pekee.
Hapo juu ni kaburi lenye mnara mrefu kuliko yote katika makumbusho ya Bagamoyo.
Mbuyu huu ni mkubwa kuliko mibuyu yote katika makumbusho ya Bagamoyo. Inasadikika kwamba ulikuwepo enzi ya utumwa.
Mamba hawa wanapatikana Bagamoyo
Hii ndio sehemu ambayo Wajerumani waliitumia kuwanyonga viongozi na wapigania haki wa Kiafrika
Subscribe to:
Posts (Atom)

