Monday, March 12, 2012

WANAFUNZI UDSM WAIENZI BAGAMOYO

 kulia ni katibu mkuu wa Accounting Association of Dar es salaam University ( AADU ) 2012, Mr Dayanus Mgaya akiwasubiri viongozi wa makumbusho ya Bagamoyo.


Sahani hiyo inaonesha vifaa mbalimbali vilivyotumika enzi ya Utumwa zikiwemo fedha na shanga. Waarabu walijenga makazi yao katika eneo hilo ambalo linajulikana kama kaole. Neno Kaole limetokana na neno la  "Chite chikalole Pumbuji" yaani twende tukaone wageni (waarabu).

Hapo juu ni wanafunzi wa kitivo cha biashara (B.COM)  Chuo kikuu Dar es salaam wakiangalia picha za ukutani zinazoonesha maajabu mbalimbali ya Bagamoyo.


Kushoto ni Mwenyekiti wa Accounting Association of Dar es salaam University, Bahati Steven akipongezana na katibu wa chama Mr. D. Mgaya.

Sanamu inayoonesha mateso makali waliyopata mababu zetu kwa kubebeshwa pembe za ndovu

Juu ni kisima cha maajabu kinachopatikana Bagamoyo, maji ya kisima hiki hayapungui wala kuongezeka katika misumu yote ya mwaka.
 Wanafunzi wakinawa maji yanayotoka katikka kisima kisichokauka. inasadikika kuwa maji haya yanabaraka za pekee.


 Hapo juu ni kaburi lenye mnara mrefu kuliko yote katika makumbusho ya Bagamoyo.
 Mbuyu huu ni mkubwa kuliko mibuyu yote katika makumbusho ya Bagamoyo. Inasadikika kwamba ulikuwepo enzi ya utumwa. 


Mamba hawa wanapatikana Bagamoyo



Hii ndio sehemu ambayo Wajerumani waliitumia kuwanyonga viongozi na wapigania haki wa Kiafrika

No comments:

Post a Comment