Sunday, March 25, 2012

MAMENEJA UDSM WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA AJIRA NCHINI.

Ikiwa ni sehemu ya agenda muhimu katika kujenga mitandao ya kijamii na kiuchumi ( networking ), wanafunzi wa Kitivo Cha Biashara wa Chuo Kikuu Dar es salaam walikutana katika ukumbi wa Mariot Hotel nje kidogo ya mji wa Mabibo kujadili masuala ya msingi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kutathimini suala la ukosefu wa ajira, fulsa za vijana kujiajiri na changamoto zilizopo katika sector ya ajira.
Wakiwa katika ukumbi wa Mariot, Mameneja hao walipata nafasi ya kujadili kwa kina umuhimu wa kuwekeza katika maarifa (elimu ) na Ushiriki katika mambo ya kijamii kwa lengo la kupata uzoefu na fikra chanya ziletazo mabadiliko (networking).
 Kwa mujibu wa LOTTU  YONA, mdau mkubwa katika mkutano huo “Wazo / idea” ni mtaji mkubwa katika utambuzi wa fulsa zilizopo ambazo kwazo vijana wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali na kuongeza nafasi za ajira nchini.
                KONAHABARI ilipata nafasi ya pekee kuwatambua washiriki wengine kutoka Ujerumani, Kenya na Uganda ambao walifurahishwa sana na juhudi za Wanafunzi wa UDSM katika masuala ya msingi ya kitaifa.

1 comment:

  1. ILIKUWA CKU NZURI SANA KWA FINALIST KWANI WATU WALIPATA ELIMU PAMOJA NA BURUDANI YA KUTOSHA MUCH RESPECT KWA BWANA CHAPPA(VENANCE) KWA KU COORDINATE MZIGO MZIMA

    ReplyDelete