Thursday, March 8, 2012

Somalia yaomba kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Somalia yaomba kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

 Somalia imetuma maombi ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali ya Kenya ilitangaza katika waraka wake siku ya Jumanne (tarehe 6 Machi)."Maombi yamefuatia maendeleo makubwa nchini Somalia ambayo yameonekana nchini kwa kuanza safari ya kujiimarisha na amani baada ya miaka mingi ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe," rais wa Kenya, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, alisema katika waraka wake.Maombi yatafikiriwa na nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Nchi zilizounda soko la pamoja mwaka 2010 na zinashughulikia kuanzisha sarafu ya pamoja mwaka huu.

No comments:

Post a Comment