Saturday, March 10, 2012

political


CHADEMA WAITIKISA ARUMERU
Chama Cha Democrasia na Maendeleo kimefanya mkutano mkubwa kama sehemu ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru mashariki. Akiongea na idadi kubwa ya watu, kamanda wa mapambano na Mwenyekiti wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) bwana Freeman Mbowe alimnadi mgombea wa Ubunge kupitia Chama chake bwana Joshua Nasari kuwa ni kijana shupavu na mwenye uwezo mkubwa wa kulinda na kutetea haki za wanyonge
Katika mkutano huo, CHADEMA iliraani vikali matumizi mabaya ya fedha za umma, rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya waandamanaji na wapigania haki nchini. imeandaliwa na konahabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment