Monday, March 19, 2012

AGOMBEA UBUNGE ALISHE FAMILIA.

Harakati za uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la Arumeru mashariki zimekuwa zikichukua taswira tofauti ambapo CCM imeonekana kupata ushindani mkubwa kutoka chama cha Democrasia na Maendeleo         ( CHADEMA ).
Akiongea na wananchi wa Arumeru mashariki Mbunge wa Mtera ( CCM ),  Livingstone Lusinde aliwaomba wananchi wa jimboi hilo kumpigia kura mgombea wa chama chake Bwana SIOI SUMARI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo  ( Jeremiah Sumari ). 
Lusinde aliitoa kauli hiyo katika kampeni za kumdadi mgombea huyo zilizofanyika katika kijiji cha Migadini, kata ya Mororoni  ambapo kiongozi huyo alitoa sababu mbalimbali za wananchi kumchagua mgombea huyo.
Lusinde alisema, wananchi wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua mgombea huyo kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara utakao muwezesha kumudu familia aliyoiacha marehemu Baba yake.
Mbunge huyo wa Mtera alienda mbali zaidi kwa kusema “mkimchagua SIOI mtapata Baraka nyingi kwa Mungu kwa kuwa mtakuwa mmemfuta machozi ya kufiwa na Baba yake, pia mtakuwa mmemfurahisha Rais kwa kuwa SIOI ndiye chaguo lake.

No comments:

Post a Comment