Thursday, March 15, 2012

MKAPA AMKANA NYERERE ARUMERU


                                            Vicent Nyerere - mbunge wa Musoma mjini ( CHADEMA )


Akizindua kampeni za CCM kwenye uwanja wa michezo wa Ngaresero, Usa River Jumatatu wiki hii, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alisema: 
“Nimefanya kazi na Mwalimu kwa miaka 25, nikiwa mwandishi wake, Waziri na katika muda huo, nimemzika yeye, kaka yake na mama yake mzazi, sijawahi kusikia jina la Vicent Nyerere kama miongoni mwa wanafamilia ya Mwl. Nyerere.
Vicent ambaye ni mbunge wa Musoma mjini kupitia Chama Cha Demorasia ( CHADEMA ) alisikitishwa sana na kauli ya Mkapa na kusema  si jambo la ajabu Mkapa kumkana yeye ( VICENT NYERERE ) kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao.
Mbunge huyo machachali wa Chadema amemtuhumu mkapa kuwa,  akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.
 Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi .
 Vicent alimtaka Mkapa kuacha kujiingiza katika masuala ya familia yao baada ya MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere 
Kwa sasa Vicent Nyerere anaendelea na kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki ambako Chadema kupitia mgombea wake Joshua Nasari anaonekana kuungwa mkono na wananchi wengi.  

No comments:

Post a Comment