Saturday, March 31, 2012

GENDER NA AMREF TANZANIA WATOA SEMINA UDSM


Gender association na AMREF TANZANIA wamefanikiwa kutoa semina juu ya mahusiano,Maambukizo ya virusi vya UKIMWI, Sheria zinazoongoza mahusiano ya kijinsia, na nafasi ya kila mwanajamii katika kajali, kuheshimu na kulinda utu na haki za Binadamu.
Semina hiyo imefanyika  leo tarehe 31/03/2012 Nyumba nambari b123 Kitivo Cha Biashara ( UDBS ) ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Chuo waliweza kuhudhuria.
Akiongea na idadi kubwa ya watu waliofika katika eneo hilo, Profesa B. KODA  kutoka ( IDS – UDSM )alitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayo wagusa Vijana katika maisha. Profesa KODA alitisha mkazo kuhusu nafasi ya Vijana kujitambua, kuitambua thamani yao na mchango wao katika jamii.
Wakisha kujitambua Vijana wanayo nafasi ya kujiepusha na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na kujihusisha katika mambo ya maendeleo. KODA amewasihi Vijana kuwa waaminifu na kutopenda starehe za muda mfupi ambazo kwazo maisha yao huharibika.
Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia KODA amezitaja sheria zinazokataza kumlazimisha mtu katika mahusiano ya kimapenzi. Hii imetoa upeo mpana zaidi kwa Vijana kuzijua sheria zinazoongoza mahusiano mema katika jamii.
                Imerekadiwa na kuletwa kwako na konahabari( blog ya kwanza kuzifikia hisia zako)
Profesa KODA akitoa semina kwa wanafunzi


No comments:

Post a Comment