Thursday, May 24, 2012

MNYIKA AWATOA WANACHADEMA KIMASOMASO, ASHINDA KESI ILIYOKUWA INAMKABILI.....



Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ),John Mnyika, ameshinda dhidi ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake wa karibu,Hawa Ng’umbi kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM). Madai yote yametupiliwa mbali na Hawa Ng’umbi ameagizwa kulipa gharama zote za uendeshwaji wa kesi hiyo
Kwa mantiki hiyo, John Mnyika ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA,anaendelea kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo - CHADEMA.

Mapokezi makubwa ya mbunge wa Ubungo- John Mnyika baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.


 

waandishi wa habari wakimpokea Mnyika baada ya kutangazwa kushinda kesi yake
John Mnyika akiwapungia mkono wananchi na wafuasi wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Kama ishara ya ushindi. 
purukushani za kiraia kushangilia ushindi wa Mnyika hazikuishia mikononi mwa Viongozi bali kwa raia wenye mapenzi mema na Chadema.
wanafunzi nao walisema hii inawahusu, suala la kuigenga nchi ni jukumu lao pia.


Sunday, May 20, 2012

CHALSEA BINGWA = AWAONDOA MUNIC FAINAL

wachezaji wa Chelsea wakifurahia kombe lao ligi kuu ya mabingwa ulaya
Drogba akimbia baada ya kufunga bao maridadi

HISIA ZA ERICK SHIGONGO

Uchu wa mapenzi ulikuwa umemjaa kupita maelezo, akili yake haikufanya kazi hata kidogo zaidi ya kuwaza jambo moja tu; kupata penzi la msichana mrembo aliyekuwa amelala kitandani huku  sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.
Wakati Jon akiwaza hayo, Theresia alikuwa usingizini tena fofofo hakuwa na shaka alimwamini Jon kuliko kitu kingine  bila kufahamu kwamba muda mchache ujao ungekuwa wa mateso kama sio maumivu.
Kazi ilikuwa imebaki moja tu; kulichomoa  taulo alilojifunga  Theresia baada ya kufanikiwa kulishusha mpaka kiunoni.
“Nitalitoa tu mpaka nifanikiwe leo ndio leo,” aliongea mzee huyo  huku akitetemeka.
Kwa takribani dakika tano nzima alibaki ameduwaa akifikiria ni nini afanye ili atakapolishusha taulo hilo Theresia asishtuke na yeye kuendelea na nia yake.
Aliunyoosha mkono na kuurudisha, akaunyoosha tena na kuurudisha, ukawa kama mchezo wa kuigiza.  Akiwa hapo akatupa macho yake kwenye saa kubwa iliyokuwa ukutani ndani ya chumba, akashuhudia saa zikiwa zimesonga mbele kuonyesha kwamba kulikuwa na saa nne tu ili mapambazuko yawadie.
“I don’t care what happens.  I will just ask her to pardon me, I hope she will understand me…”  (Potelea mbali na kitakachotokea.  Nitamwomba anisamehe, ninatumaini atanielewa…”)
 “One! Two! Thre..? (Moja! Mbili, Tat…) akashindwa kumalizia sentensi yake, kwa nguvu akalikamata taulo  na kuanza kulivuta.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Hakuweza kutimiza lengo lake alipofikisha tatu, huku akitetemeka akalivuta taulo kwa nguvu bila kuelewa kwamba jambo hilo lingemshtua Theresia kutoka katika usingizi aliokuwa amelala na kumwamsha.
“Cosa è successo?” (Nini kimetokea?) aliuliza Theresia kwa  sauti huku akikurupuka kutoka kitandani na kusimama wima, chini macho yake yote yakimwangalia Jon na  kushuhudia akiwa mtupu kama alivyozaliwa,  mkononi mwake akiwa na taulo ambalo  Theresia alijifunga muda mchache kabla ya kupanda kitandani.

Akiwa haelewi ni kitu gani kimetokea akazungusha macho yake huku na kule ndani ya chumba na kutua juu ya mwili wake naye alikuwa amebaki mtupu kama alivyozaliwa, huku akilia, haraka akakisogelea kitanda na kulivuta shuka lililokuwa juu yake na kujifunika.
“Jon!” Theresia aliita.
“Mh!”
“Che cosa è questo?”(Kuna nini tena?) aliuliza Theresia kwa lugha ya Kiitaliano  akimshuhudia pia Jon akiwa mtupu kama alivyozaliwa na sehemu zake za mbele zikiwa zimetuna
 “Vuoi fare? (Unataka kufanya nini?)
“Mh!” bado aliendelea kukataa kwa kutingisha kichwa, alikuwa amepatwa na kigugumizi cha ghafla, uchu wote wa penzi aliokuwa nao ulitoweka kama upepo.
“Dov’è il mio asciugamano? Perché ho ragione?”(Taulo langu liko wapi? Kwa nini niko hivi?)
Jon hakuweza kujibu kitu  akiwa hapo akaizungusha akili yake akitafuta uongo ambao ungetosheleza kumweleza Theresia ili kuficha ukweli wa jambo alilokuwa akitaka kulifanya usiku huo.
“Perchè non sei? (Kwa nini na wewe uko hivyo?) aliuliza Theresia huku akibubujikwa na machozi.
“Si tratta di un brutto sogno che anche io non posso dire”  (Ni ndoto mbaya ambayo hata mimi siwezi kuisimulia.)
“Per me e si dispone di un vuoto?”(Ya mimi na wewe kuwa utupu?)
Kigugumizi kikamkamata Jon, hakuwa na jibu la kumpa Theresia, akainamisha kichwa chake chini na kuanza kulia  machozi,  ndani ya moyo wake akijilaumu kuchukua uamuzi ambao sasa ulikuwa ukimweka matatizoni,  akiwa hapo  akamshuhudia Theresia akichukua nguo zake na kuvaa huku akilia, akijuta kukuta na Jon, mwanaume aliyemwamini  kwa dhati lakini sasa alikuwa amemtenda mabaya.
Alipomaliza kuvaa nguo zake akamgeukia Jon na kumwambia wazi kwamba alikuwa akiondoka na tangu siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wa penzi lao  na kamwe asijaribu kumtafuta kwa lolote na kama ni zawadi zake alizompa basi angezirejesha ili awe huru.
“Hapana Theresia, ninakupenda ni shetani tu alinipitia akanidanganya na sasa najuta!”
“Ungekuwa unanipenda kwa dhati Jon ungesubiri mpaka tufunge ndoa  ili iwe na baraka lakini sasa umeharibu kwa kuniingilia kimwili bila ridhaa yangu…mimi ninaondoka nakwenda…” aliongea Theresia muda wote huo akibubujikwa na machozi.
“Naapa kwa Mungu sijafanya kitu chochote, nilikuwa nataka kufany…” alisema huku akiwa amepiga magoti chini kuomba msamaha.
“Hapana Jon ninaondoka, nakuacha na mali zako, utapata mwanamke mwingine ambaye utamuoa lakini mimi siko tayari.”
“Tafadhali Theresia rudi kwangu, wewe ndiyo mke wangu  wa maisha mama wa watoto wangu!”
“Nasema hapana, tafadhali niache niende zangu.”
“Lakini hivi sasa ni usiku tena mkubwa utaondokaje?”
”Nitalala nje ya nyumba yako mpaka mapambazuko nitajua tu jinsi ya kuondoka, Jon ahsante kwa kila kitu.”
“Theresia ukiniacha ninakuhakikishia nitajiua.”
“Unachekesha kweli wewe ujiue kwa sababu ya mwanamke? Mbona wapo wengi wazuri Jon hebu niachie niondoke.”
“Siko tayari, nasema siko tayari kukuacha uende.”
“Ni kwa nini ulitaka kunibaka?”
“Tamaa ya mwili ndiyo iliyopelekea yote hayo lakini ninakuomba unisamehe, niko tayari kukupatia nusu ya utajiri wangu  lakini tu unipe msamaha wako mpenzi wangu…”
“Basi baki na tamaa zako mimi nakwenda zangu,” aliongea Theresia na kujifyatua mikononi mwa Jon, haraka akakimbia kuuelekea mlango kisha kuukamata, na kwa macho yake yote mawili akamwona akiufungua na kutoka nje.
“Theresia non mi abbandonare io ti amo, sicuramente ho giurato che mi sono suicidato, non a lungo termine.”(Theresia usiniache ninakupenda, hakika ninakuapia nitajiua muda si mrefu) alipaza sauti ambayo ilimshtua Theresia kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala.
“Jon!” aliita Theresia akinyanyuka kutoka kitandani na kuketi kitako.
Akamshuhudia Jon Curtis akitetemeka, jasho jingi likitiririka mwilini mwake, mapigo yake ya moyo nayo yalikwenda mbio mithili ya  mtu aliyekimbia mbio ndefu,  Theresia akahisi tatizo kubwa lilikuwa limetokea, bila kusema kitu chochote  Jon akamsogelea Theresia na kumkumbatia kwa nguvu.
“Si tratta di un brutto sogno”(Ni ndoto mbaya) aliongea Jon huku akitetemeka.
Hakika ilikuwa ni ndoto mbaya katika zote alizowahi kuota mwanaume huyo, kitendo cha kushuhudia Theresia akiondoka na kumweleza wazi kwamba katika maisha yake asahau kuonana naye tena, kiliuumiza moyo wake.
“Pole mpenzi wangu hebu nieleze umeota nini?”
“Nimeota umeniacha.”
“Mh!” aliguna Theresia na wote wawili wakaachia kicheko.
Tayari mapambazuko yalishawadia hivyo hawakuona haja ya kulala  zaidi ya kuendelea  kuongea huku Theresia akijaribu kumtuliza Jon ambaye mpaka wakati huo bado hakuwa akiamini alichokishuhudia ndani ya ndoto yake.
“Jon! Tayari ni mapambazuko ni vyema tukajiandaa ili mimi niwahi kazini na kufanya ule mchakato wa kuongea na baba.”
“Itakuwa imesaidia sana ndoto hii niliyoota, hakika inamenitia shaka nahisi kukukosa muda si mrefu.”
“Mimi ni wako daima,” aliongea Theresia huku akinyanyuka kitandani, akatembea kuelekea bafuni kwa ajili ya kuoga na kujiandaa.
“Siku zote nitakupenda,” Jon aliongea huku akikodoa macho yake kumwangalia Theresia.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatano katika gazeti la Risasi Mchanganyiko.

Thursday, May 17, 2012

NAFASI ZA KAZI.........

 
Kampuni ya CHIWACO INVESTMENT'S COMPANY LIMITED.
inatangaza nafas ya kaz katika mgodi mpya MASUMBWE BUKOMBE

1) Operators nafasi 14
2) Supervisors nafasi 17
3) Ofisi secretary nafasi 10
4) madereva wa magari nafasi 14

mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28/5/2012 tuma kwa email vivul vya kopi za elimu au uzoefu wa kazi
meneja uhusiano.

email chiwainvestment@gmail.com
au piga simu muda wa kazi 0769560479

YALIYOJILI BAADA YA KIFO CHA PATRICK MAFISANGO - ALIYEKUWA MCHEZAJI WA SIMBA.

Aliyekua kiungo mkabaji wa Klabu ya Simba Ptrick Mafisango akirushwa juu katika moja ya mechi baada ya kufunga bao wakati wa Uhai wake.

Patrick Mutesa Mafisango alipata ajali saa 9:00 usiku kwenye eneo la Veta na kufariki dunia. Kufuatia kifo hicho rafiki yake mkubwa, Haruna Moshi Boban ameshindwa kuhudhuria mazoezi ya timu ya Taifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam."Alikua akikwepa mtu mwenye baiskeli baada ya kuingia barabarani ghafla wakati gari ikiwa kwenye spidi likamshinda ndipo lilipo tumbukia kwenye mtaro," alisema mmoja ya abiria aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Mchezaji haruna Niyonzima wa Yanga, Pawasa amesema jana walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati bendi ya Akudo Impact ikifanya onyesho klabuni hapo na marehemu alimuaga kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu akiambiwa mwenye simu hii amefariki dunia kwa ajali.

Haruna Moshi Boban akibembelezwa baada ya kutoka kuona mwili wa Rafikiyake marehemu Patrick Mutesa Mafisango kwenye Chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Monday, May 14, 2012

UDBS TIMU YAGEUKA TISHIO SAYONA CUP, YAICHAPA COECT BAADA YA CASS.YAONGOZA KUNDI LAKE KWA USHINDI MNONO....

Timu ya UDBS imeendeleza wimbi lake la ushindi mwishoni mwa wiki hii baada ya kuichapa bila huruma timu ya COECT jumla ya mabao manne kwa mawili katika Kombe la Sayona ( Sayona CUP ) Uwanja wa Mabibo hostel.
UDBS timu ambayo imeonekana kuwa tishio katika michuano hiyo iliingia uwanjani ikiwa na rekodi ya Ushindi wa mabao mawili kwa bila iliyo upata katika mechi ya kwanza dhidi ya CASS mwishoni mwa wiki iliyopita. Ikiongozwa na Washambuliaji machachali na vijana wenye uzoefu katika michuano mikubwa, UDBS ilifanikiwa kujipatia mabao yote manne katika dakika arobaini na tano ( 45 ) za kipindi cha kwanza huku COECT wakiambulia goli moja tu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu ambapo UDBS walionekana kumiliki zaidi safu ya ushambuliaji huku COECT wakijihami na kupanda mbele kwa tahadhari kubwa. Uchu wa kulizamisha zaidi jahazi la COECT uliiponza UDBS dakika ya sitini na mbili ya mchezo ambapo UDBS walijenga kambi langoni mwa COECT na kuisahau safu ya ulinzi ambayo ilitumiwa vizuri na COECT kujipatia bao la pili.
Piga nikupige langoni mwa COECT haikuisha hadi dakika ya tisini ya mchezo ambayo iliamua ushindi ya bao NNE ( 4 ) kwa UDBS na COECT bao mbili ( 2 ). Kwa ushindi huo UDBS imejikusanyia jumla ya point 6 na mabao 6 hivyo kuongoza katika kundi lake.
Mechi nyingine zinaendelea kupingwa katika uwanja wa mabibo kama hatua muhimu za kufuzu kuelekea fainali za Sayona CUP msimu huu.
konahabari haikufanikiwa kupiga picha katika mechi kutokana na hali mbaya ya hewa iliyoambatana na mvua....

Wednesday, May 9, 2012

MAMENEJA-UDSM KUKUTANA KWA CHAKULA CHA PAMOJA HOTEL YA KIFAHARI....

Mameneja - Mwaka wa tatu, kitivo cha Bishara Chuo Kikuu Dar es salaam ( B.COM ) wamepanga kukutana kwa Chakula cha pamoja ( CORPORATE DINNER ) katika Hotel ya kifahari ya MALLIOTE nje kidogo ya mji wa Mabibo.
Wakiongea na Konahabari jana  ( nje ya Cafteria 2 Campus ya mwl. Nyerere - Chuo Kikuu Dar es salaam ) waandaaji wa chakula hicho cha jioni walizungumzia umuhimu wa kukutana pamoja na kujadili mambo ya msingi yanayoigusa jamii kwa namna mbalimbali.
Kwa mujibu wa Paul Venance, mjumbe katika kamati kuu ya uandaaji wa Chakula hicho; Mkutano huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wale watakao pata nafasi ya kuhudhia. 
" Hii ndiyo sehemu pekee ambayo mameneja watapata fulsa ya kubadilisha uzoefu na kupeana mikakati yakinifu katika kuzitambua na kuzitumia fulsa zilizopo. Ni sehemu ya kupeana taswira ya soko la ajira na mbinu za kuukabili ushindani wa kibiashara" Alisema Venance.
Corporate Dinner kwa upande mwingine, imetafsiliwa na baadhi ya wadau kama silaha muhimu ya watu kufahamiana na kujenga undugu ambao ndio falsafa mama ya jamii yoyete iliyostaarabika duniani. 
Wadau wanaendelea kutoa michango yao kwa Viongozi - wanakamati walioidhinishwa kisheria kuipokea michango hiyo. SHILINGI ELFU KUMI TU ( 10,000 only ).. ya Kitanzania itamtosha kila Meneja atakaye shiriki katika Corporate dinner kuweza kula, kunywa, kuburudika kwa michezo mbalimbali na kuelimika katika mtazamo wa kimeneja.
Hii Sio ya kukosa, 
                   
PIGA : 0717 438 287            KUWASILISHA MCHANGO WAKO
                                                    WOTE   MNAKARIBISHWA !

Sunday, May 6, 2012

SIMBA AMLA MWANA WA JANGWANI UWANJA WA TAIFA

Mechi ya Kuwania ubingwa wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara imemalizika dakika chache zilizopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika hali isiyoaminika Timu ya SIMBA imefanikiwa kuifunga YANGA kwa jumla ya bao 5 bila kelele.
SIMBA imetoa adhabu hiyo kali kwa YANGA ikiwa ni sehemu muhimu na pekee ya kudhihirisha ubingwa wake ambao ilifahamika hata kabla ya mchezo wa leo.Rekodi nzuri ya SIMBA katika mechi za ndani na kimataifa inatoa kibari kwa washabiki na wapenzi wa Msimbazi kuimiliki furaha ya mchezo msimu huu.
washabiki wa SIMBA wakiwa na furaha kubwa.....
                    na mwandishi wa konahabari uwanja wa taifa.....

Saturday, May 5, 2012

TIMU YA UDBS YAANZA VIZURI KWA KUICHAPA CASS BAO MBILI KWA NUNGE (SAYONA CUP UWANJA WA MABIBO HOSTEL.)

Timu ya mpira wa miguu ya UDBS( University of Dar es salaam Business School ) imeanza vema michuano ya SAYONA CUP iliyoandaliwa na watengenezaji wa kinywaji SAYONA baada ya kufanikiwa kuiadhibu bila huruma timu ya CASS kwa jumla ya bao mbili bila majibu.
Katika dakika zote tisini za mchezo, UDBS walionekana kuutawala mpira na kupelekea amsha amsha za hapa na pale katika lango la CASS.
Juhudi za CASS Kulinda lango lao lisiweze kutikiswa na UDBS zilishindwa mapema mwanzoni mwa kipindi cha kwanza ambapo UDBS walifanikiwa kujipatia goli safi na kuamsha hisia za ushindi.
Dakika 45 za kipindi cha pili ziliwatosha UDBS na wala sio CASS kupachika bao la pili. Bao hili lilifungwa na mshambuliaji machachali wa UDBS ( Carlic ) na kufunga ukurasa  wa mabao katika mechi hiyo
Konahabari ilifanikiwa kurekodi jumla ya magoli mawili kwa UDBS na kushindwa kuandika chochote kwa CASS mpaka dakika ya 90. Michuano hiyo inaendelea katika uwanja wa mabibo ambapo timu nyingine zinaendelea kurusha karata zao.
kikosi cha UDBS kilicho iadhibu CASS ( 2-0 )
Kikosi cha CASS kilicho fungwa bao 2 na UDBS.

AIESEC UDSM YAFANYA KONGAMANO KUBWA NKURUMAH HALL

 
AIESEC - UDSM ( University of Dar es salaam ) imefanikiwa kufanya mkutano mkubwa na wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali, Makampuni, taasisi na waandishi wa habari. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine AIESEC wameeleza umuhimu wa Vijana kuendeleza taaluma zao kama dira muhimu ya jamii kujitambua, kutambua fulsa zilizopo na hatimaye kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.
Mkutano wa AIESEC - UDSM umedhaminiwa na makampuni mbalimbali ambayo yanautambua mchango wa AESEC katika maendeleo ya vijana. Miongoni mwa makampuni hayo ni Cocacola, CRDB,TIGO NA TWIGA CEMENT
Licha ya hatua kubwa iliyofikiwa na AIESEC bado kuna umuhimu wa Vijana wengi kuijua na kuutambua mchango wa AEISEC katika jamii kama makampuni yaitambuavyo AEISEC.
Hii ni historia fupi ya AIESEC.
Wazo kuu kuhusu AIESEC lilianza katika miaka ya 1930, wakati wawakilishi kutoka shule za Ulaya walipokuwa wakibadilishana habari kuhusu mipango tofauti na shule maalumu katika biashara na uchumi.
Shughuli rasmi za "kusaidia kuendeleza 'mahusiano ya kirafiki' kati ya nchi wanachama" yalianza mwaka 1946, na AIESEC kwa mara ya kwanza ilianzishwa rasmi mwaka 1948. Wakati huo, misheni ilikuwa "kupanua uelewa wa watu, kubadilisha ulimwengu kwa mtu mmoja kwa wakati.
Mwaka 1949, wanafunzi 89 walishiriki katika iliyoitwa "Stockholm Congress ", iliyokuwa ya kwanza kati ya "Programu za Kubadilishana wanafunzi". Ndani ya mda mfupi, AIESEC ikawa maarufu.
Hatua kubwa katika historia ya AIESEC ilikuja wakati "Dhima ya programu ya kimataifa" ilipoanzisha rasmi semina za kimataifa, kikanda, na mitaa kuhusu mada maalumu, ambayo baada ya mda ilikuwa na kuwa mwongozo wa AIESEC kwa vizazi vilivofuata baadaye. Katika miongo iliyofuata, mada za majadiliano zilikuwa Biashara za Kimataifa, Elimu ya Manejimenti, maendeleo endelevu, Ujasiliamali na Majukumu ya Ushirika, na katika miaka ya 1990, mtandao wa ndani ulioitwa Insight ulianzishwa kuwezesha mitandao.