Monday, May 14, 2012

UDBS TIMU YAGEUKA TISHIO SAYONA CUP, YAICHAPA COECT BAADA YA CASS.YAONGOZA KUNDI LAKE KWA USHINDI MNONO....

Timu ya UDBS imeendeleza wimbi lake la ushindi mwishoni mwa wiki hii baada ya kuichapa bila huruma timu ya COECT jumla ya mabao manne kwa mawili katika Kombe la Sayona ( Sayona CUP ) Uwanja wa Mabibo hostel.
UDBS timu ambayo imeonekana kuwa tishio katika michuano hiyo iliingia uwanjani ikiwa na rekodi ya Ushindi wa mabao mawili kwa bila iliyo upata katika mechi ya kwanza dhidi ya CASS mwishoni mwa wiki iliyopita. Ikiongozwa na Washambuliaji machachali na vijana wenye uzoefu katika michuano mikubwa, UDBS ilifanikiwa kujipatia mabao yote manne katika dakika arobaini na tano ( 45 ) za kipindi cha kwanza huku COECT wakiambulia goli moja tu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu ambapo UDBS walionekana kumiliki zaidi safu ya ushambuliaji huku COECT wakijihami na kupanda mbele kwa tahadhari kubwa. Uchu wa kulizamisha zaidi jahazi la COECT uliiponza UDBS dakika ya sitini na mbili ya mchezo ambapo UDBS walijenga kambi langoni mwa COECT na kuisahau safu ya ulinzi ambayo ilitumiwa vizuri na COECT kujipatia bao la pili.
Piga nikupige langoni mwa COECT haikuisha hadi dakika ya tisini ya mchezo ambayo iliamua ushindi ya bao NNE ( 4 ) kwa UDBS na COECT bao mbili ( 2 ). Kwa ushindi huo UDBS imejikusanyia jumla ya point 6 na mabao 6 hivyo kuongoza katika kundi lake.
Mechi nyingine zinaendelea kupingwa katika uwanja wa mabibo kama hatua muhimu za kufuzu kuelekea fainali za Sayona CUP msimu huu.
konahabari haikufanikiwa kupiga picha katika mechi kutokana na hali mbaya ya hewa iliyoambatana na mvua....

1 comment:

  1. Managers huwa wanatisha wakati wote na mahali popote! Great and big up ...............

    ReplyDelete