Saturday, May 5, 2012

AIESEC UDSM YAFANYA KONGAMANO KUBWA NKURUMAH HALL

 
AIESEC - UDSM ( University of Dar es salaam ) imefanikiwa kufanya mkutano mkubwa na wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali, Makampuni, taasisi na waandishi wa habari. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine AIESEC wameeleza umuhimu wa Vijana kuendeleza taaluma zao kama dira muhimu ya jamii kujitambua, kutambua fulsa zilizopo na hatimaye kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.
Mkutano wa AIESEC - UDSM umedhaminiwa na makampuni mbalimbali ambayo yanautambua mchango wa AESEC katika maendeleo ya vijana. Miongoni mwa makampuni hayo ni Cocacola, CRDB,TIGO NA TWIGA CEMENT
Licha ya hatua kubwa iliyofikiwa na AIESEC bado kuna umuhimu wa Vijana wengi kuijua na kuutambua mchango wa AEISEC katika jamii kama makampuni yaitambuavyo AEISEC.
Hii ni historia fupi ya AIESEC.
Wazo kuu kuhusu AIESEC lilianza katika miaka ya 1930, wakati wawakilishi kutoka shule za Ulaya walipokuwa wakibadilishana habari kuhusu mipango tofauti na shule maalumu katika biashara na uchumi.
Shughuli rasmi za "kusaidia kuendeleza 'mahusiano ya kirafiki' kati ya nchi wanachama" yalianza mwaka 1946, na AIESEC kwa mara ya kwanza ilianzishwa rasmi mwaka 1948. Wakati huo, misheni ilikuwa "kupanua uelewa wa watu, kubadilisha ulimwengu kwa mtu mmoja kwa wakati.
Mwaka 1949, wanafunzi 89 walishiriki katika iliyoitwa "Stockholm Congress ", iliyokuwa ya kwanza kati ya "Programu za Kubadilishana wanafunzi". Ndani ya mda mfupi, AIESEC ikawa maarufu.
Hatua kubwa katika historia ya AIESEC ilikuja wakati "Dhima ya programu ya kimataifa" ilipoanzisha rasmi semina za kimataifa, kikanda, na mitaa kuhusu mada maalumu, ambayo baada ya mda ilikuwa na kuwa mwongozo wa AIESEC kwa vizazi vilivofuata baadaye. Katika miongo iliyofuata, mada za majadiliano zilikuwa Biashara za Kimataifa, Elimu ya Manejimenti, maendeleo endelevu, Ujasiliamali na Majukumu ya Ushirika, na katika miaka ya 1990, mtandao wa ndani ulioitwa Insight ulianzishwa kuwezesha mitandao.1 comment:

  1. it was real awesome moment for the university student to meet their prospect employee

    ReplyDelete