Saturday, May 5, 2012

TIMU YA UDBS YAANZA VIZURI KWA KUICHAPA CASS BAO MBILI KWA NUNGE (SAYONA CUP UWANJA WA MABIBO HOSTEL.)

Timu ya mpira wa miguu ya UDBS( University of Dar es salaam Business School ) imeanza vema michuano ya SAYONA CUP iliyoandaliwa na watengenezaji wa kinywaji SAYONA baada ya kufanikiwa kuiadhibu bila huruma timu ya CASS kwa jumla ya bao mbili bila majibu.
Katika dakika zote tisini za mchezo, UDBS walionekana kuutawala mpira na kupelekea amsha amsha za hapa na pale katika lango la CASS.
Juhudi za CASS Kulinda lango lao lisiweze kutikiswa na UDBS zilishindwa mapema mwanzoni mwa kipindi cha kwanza ambapo UDBS walifanikiwa kujipatia goli safi na kuamsha hisia za ushindi.
Dakika 45 za kipindi cha pili ziliwatosha UDBS na wala sio CASS kupachika bao la pili. Bao hili lilifungwa na mshambuliaji machachali wa UDBS ( Carlic ) na kufunga ukurasa  wa mabao katika mechi hiyo
Konahabari ilifanikiwa kurekodi jumla ya magoli mawili kwa UDBS na kushindwa kuandika chochote kwa CASS mpaka dakika ya 90. Michuano hiyo inaendelea katika uwanja wa mabibo ambapo timu nyingine zinaendelea kurusha karata zao.
kikosi cha UDBS kilicho iadhibu CASS ( 2-0 )
Kikosi cha CASS kilicho fungwa bao 2 na UDBS.

No comments:

Post a Comment