Sunday, May 20, 2012

HISIA ZA ERICK SHIGONGO

Uchu wa mapenzi ulikuwa umemjaa kupita maelezo, akili yake haikufanya kazi hata kidogo zaidi ya kuwaza jambo moja tu; kupata penzi la msichana mrembo aliyekuwa amelala kitandani huku  sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.
Wakati Jon akiwaza hayo, Theresia alikuwa usingizini tena fofofo hakuwa na shaka alimwamini Jon kuliko kitu kingine  bila kufahamu kwamba muda mchache ujao ungekuwa wa mateso kama sio maumivu.
Kazi ilikuwa imebaki moja tu; kulichomoa  taulo alilojifunga  Theresia baada ya kufanikiwa kulishusha mpaka kiunoni.
“Nitalitoa tu mpaka nifanikiwe leo ndio leo,” aliongea mzee huyo  huku akitetemeka.
Kwa takribani dakika tano nzima alibaki ameduwaa akifikiria ni nini afanye ili atakapolishusha taulo hilo Theresia asishtuke na yeye kuendelea na nia yake.
Aliunyoosha mkono na kuurudisha, akaunyoosha tena na kuurudisha, ukawa kama mchezo wa kuigiza.  Akiwa hapo akatupa macho yake kwenye saa kubwa iliyokuwa ukutani ndani ya chumba, akashuhudia saa zikiwa zimesonga mbele kuonyesha kwamba kulikuwa na saa nne tu ili mapambazuko yawadie.
“I don’t care what happens.  I will just ask her to pardon me, I hope she will understand me…”  (Potelea mbali na kitakachotokea.  Nitamwomba anisamehe, ninatumaini atanielewa…”)
 “One! Two! Thre..? (Moja! Mbili, Tat…) akashindwa kumalizia sentensi yake, kwa nguvu akalikamata taulo  na kuanza kulivuta.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Hakuweza kutimiza lengo lake alipofikisha tatu, huku akitetemeka akalivuta taulo kwa nguvu bila kuelewa kwamba jambo hilo lingemshtua Theresia kutoka katika usingizi aliokuwa amelala na kumwamsha.
“Cosa è successo?” (Nini kimetokea?) aliuliza Theresia kwa  sauti huku akikurupuka kutoka kitandani na kusimama wima, chini macho yake yote yakimwangalia Jon na  kushuhudia akiwa mtupu kama alivyozaliwa,  mkononi mwake akiwa na taulo ambalo  Theresia alijifunga muda mchache kabla ya kupanda kitandani.

Akiwa haelewi ni kitu gani kimetokea akazungusha macho yake huku na kule ndani ya chumba na kutua juu ya mwili wake naye alikuwa amebaki mtupu kama alivyozaliwa, huku akilia, haraka akakisogelea kitanda na kulivuta shuka lililokuwa juu yake na kujifunika.
“Jon!” Theresia aliita.
“Mh!”
“Che cosa è questo?”(Kuna nini tena?) aliuliza Theresia kwa lugha ya Kiitaliano  akimshuhudia pia Jon akiwa mtupu kama alivyozaliwa na sehemu zake za mbele zikiwa zimetuna
 “Vuoi fare? (Unataka kufanya nini?)
“Mh!” bado aliendelea kukataa kwa kutingisha kichwa, alikuwa amepatwa na kigugumizi cha ghafla, uchu wote wa penzi aliokuwa nao ulitoweka kama upepo.
“Dov’è il mio asciugamano? Perché ho ragione?”(Taulo langu liko wapi? Kwa nini niko hivi?)
Jon hakuweza kujibu kitu  akiwa hapo akaizungusha akili yake akitafuta uongo ambao ungetosheleza kumweleza Theresia ili kuficha ukweli wa jambo alilokuwa akitaka kulifanya usiku huo.
“Perchè non sei? (Kwa nini na wewe uko hivyo?) aliuliza Theresia huku akibubujikwa na machozi.
“Si tratta di un brutto sogno che anche io non posso dire”  (Ni ndoto mbaya ambayo hata mimi siwezi kuisimulia.)
“Per me e si dispone di un vuoto?”(Ya mimi na wewe kuwa utupu?)
Kigugumizi kikamkamata Jon, hakuwa na jibu la kumpa Theresia, akainamisha kichwa chake chini na kuanza kulia  machozi,  ndani ya moyo wake akijilaumu kuchukua uamuzi ambao sasa ulikuwa ukimweka matatizoni,  akiwa hapo  akamshuhudia Theresia akichukua nguo zake na kuvaa huku akilia, akijuta kukuta na Jon, mwanaume aliyemwamini  kwa dhati lakini sasa alikuwa amemtenda mabaya.
Alipomaliza kuvaa nguo zake akamgeukia Jon na kumwambia wazi kwamba alikuwa akiondoka na tangu siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wa penzi lao  na kamwe asijaribu kumtafuta kwa lolote na kama ni zawadi zake alizompa basi angezirejesha ili awe huru.
“Hapana Theresia, ninakupenda ni shetani tu alinipitia akanidanganya na sasa najuta!”
“Ungekuwa unanipenda kwa dhati Jon ungesubiri mpaka tufunge ndoa  ili iwe na baraka lakini sasa umeharibu kwa kuniingilia kimwili bila ridhaa yangu…mimi ninaondoka nakwenda…” aliongea Theresia muda wote huo akibubujikwa na machozi.
“Naapa kwa Mungu sijafanya kitu chochote, nilikuwa nataka kufany…” alisema huku akiwa amepiga magoti chini kuomba msamaha.
“Hapana Jon ninaondoka, nakuacha na mali zako, utapata mwanamke mwingine ambaye utamuoa lakini mimi siko tayari.”
“Tafadhali Theresia rudi kwangu, wewe ndiyo mke wangu  wa maisha mama wa watoto wangu!”
“Nasema hapana, tafadhali niache niende zangu.”
“Lakini hivi sasa ni usiku tena mkubwa utaondokaje?”
”Nitalala nje ya nyumba yako mpaka mapambazuko nitajua tu jinsi ya kuondoka, Jon ahsante kwa kila kitu.”
“Theresia ukiniacha ninakuhakikishia nitajiua.”
“Unachekesha kweli wewe ujiue kwa sababu ya mwanamke? Mbona wapo wengi wazuri Jon hebu niachie niondoke.”
“Siko tayari, nasema siko tayari kukuacha uende.”
“Ni kwa nini ulitaka kunibaka?”
“Tamaa ya mwili ndiyo iliyopelekea yote hayo lakini ninakuomba unisamehe, niko tayari kukupatia nusu ya utajiri wangu  lakini tu unipe msamaha wako mpenzi wangu…”
“Basi baki na tamaa zako mimi nakwenda zangu,” aliongea Theresia na kujifyatua mikononi mwa Jon, haraka akakimbia kuuelekea mlango kisha kuukamata, na kwa macho yake yote mawili akamwona akiufungua na kutoka nje.
“Theresia non mi abbandonare io ti amo, sicuramente ho giurato che mi sono suicidato, non a lungo termine.”(Theresia usiniache ninakupenda, hakika ninakuapia nitajiua muda si mrefu) alipaza sauti ambayo ilimshtua Theresia kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala.
“Jon!” aliita Theresia akinyanyuka kutoka kitandani na kuketi kitako.
Akamshuhudia Jon Curtis akitetemeka, jasho jingi likitiririka mwilini mwake, mapigo yake ya moyo nayo yalikwenda mbio mithili ya  mtu aliyekimbia mbio ndefu,  Theresia akahisi tatizo kubwa lilikuwa limetokea, bila kusema kitu chochote  Jon akamsogelea Theresia na kumkumbatia kwa nguvu.
“Si tratta di un brutto sogno”(Ni ndoto mbaya) aliongea Jon huku akitetemeka.
Hakika ilikuwa ni ndoto mbaya katika zote alizowahi kuota mwanaume huyo, kitendo cha kushuhudia Theresia akiondoka na kumweleza wazi kwamba katika maisha yake asahau kuonana naye tena, kiliuumiza moyo wake.
“Pole mpenzi wangu hebu nieleze umeota nini?”
“Nimeota umeniacha.”
“Mh!” aliguna Theresia na wote wawili wakaachia kicheko.
Tayari mapambazuko yalishawadia hivyo hawakuona haja ya kulala  zaidi ya kuendelea  kuongea huku Theresia akijaribu kumtuliza Jon ambaye mpaka wakati huo bado hakuwa akiamini alichokishuhudia ndani ya ndoto yake.
“Jon! Tayari ni mapambazuko ni vyema tukajiandaa ili mimi niwahi kazini na kufanya ule mchakato wa kuongea na baba.”
“Itakuwa imesaidia sana ndoto hii niliyoota, hakika inamenitia shaka nahisi kukukosa muda si mrefu.”
“Mimi ni wako daima,” aliongea Theresia huku akinyanyuka kitandani, akatembea kuelekea bafuni kwa ajili ya kuoga na kujiandaa.
“Siku zote nitakupenda,” Jon aliongea huku akikodoa macho yake kumwangalia Theresia.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatano katika gazeti la Risasi Mchanganyiko.

No comments:

Post a Comment