Thursday, May 24, 2012

MNYIKA AWATOA WANACHADEMA KIMASOMASO, ASHINDA KESI ILIYOKUWA INAMKABILI.....Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ),John Mnyika, ameshinda dhidi ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake wa karibu,Hawa Ng’umbi kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM). Madai yote yametupiliwa mbali na Hawa Ng’umbi ameagizwa kulipa gharama zote za uendeshwaji wa kesi hiyo
Kwa mantiki hiyo, John Mnyika ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA,anaendelea kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo - CHADEMA.

Mapokezi makubwa ya mbunge wa Ubungo- John Mnyika baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.


 

waandishi wa habari wakimpokea Mnyika baada ya kutangazwa kushinda kesi yake
John Mnyika akiwapungia mkono wananchi na wafuasi wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Kama ishara ya ushindi. 
purukushani za kiraia kushangilia ushindi wa Mnyika hazikuishia mikononi mwa Viongozi bali kwa raia wenye mapenzi mema na Chadema.
wanafunzi nao walisema hii inawahusu, suala la kuigenga nchi ni jukumu lao pia.


No comments:

Post a Comment