Saturday, March 17, 2012

Marketing forum na mtazamo wa Vijana kujiajiri.

 ukumbi wa Nkurumah wa chuo kikuu Dar es salaam

 Wanafunzi na Wageni wakiandikisha ili kuingia katika ukumbi wa Nkurumah siku ya Marketing Forum 17/03/2012
 IKUCHUKWU akitoa somo
 Mahojiano ndani ya Nkurumah

 Mwakilishi wa Azania Bank

 Erick Tafisa akihojiwa na waandishi wa habari

 Saa ya Chakula siku ya marketing forum


IKUCHUKWU akijibu maswali ya Vijana, full story

Dar es salaam University Marketing Association ( DUMA ) imefanya kongamano kubwa na waandishi wa habari, makampuni, taasisi za kiraia na wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali nchini. Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Nkurumah wa  Chuo Kikuu Dar es saalam.
Maada kuu katika kongamano hilo ni nafasi ya Vijana kujiajiri, ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa ziuzikazo katika masoko na uendelezaji wa taaluma za wasomi ili kuyafikia mafanikio ya kweli.
                Watoa maada wakuu  katika kongamano hilo ni pamoja na IKUCHUKWU KALU- Mtaalamu wa masoko ya ndani na nje ya nchi na IMANI KAJULA – Director wa masoko Benki ya NMB.
                Kongamano hilo limeanza saa tatu asubuhi ambapo Viongozi,wanachama wa DUMA na wageni kutoka maeneo mbalimbali walikusanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es salaam huku wakiwa na shauku kubwa ya  kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo masoko na fulsa zilizopo katika soko la ajira.
                Mwenyekiti wa DUMA, Mr. Frank Minazi ambaye ni Mwanafunzi wa kitivo cha Biashara idara ya masoko Chuo kikuu Dar es salaam alifungua kongamano kwa kuwakaribisha wageni waalikwa na wote waliohudhulia. Baada ya utambulisho wa kiitifaki, mwenyekiti alimkaribisha IMANI KAJULA kutoa maada kwa mamia ya watu waliokuwapo Nkurumah.
                KAJULA akiutumia vizuri uzoefu wake katika masoko alifanikiwa kuyaweka bayana mambo ya msingi katika kuyafikia malengo, ikiwa ni pamoja na kujiamini kujituma katika kazi, ubunifu na uwajibikaji. Hakusita pia kuelezea umuhimu wa makampuni, taasisi na watu kujijengea imani na jamii wateja wao. Neno hili aliliita ( BRANDING ). Kwa mujibu wa Kajula, mtu anaye kuwa na sifa nzuri katika jamii, Taswira ( image ) yake ni rasilimali.
                IKECHUKWU KALU, kwa upande wake alijikita zaidi kuelezea nafasi ya Vijana kujiajiri. Mtoa maada alianza kwa kukili kuwa “ Ipo nafasi ya Vijana kujiajiri” mtazamo thabiti ( VISION ) na malengo  ya muda mrefu ni silaha muhimu katika kujiajiri, “alisema KALU”. Endapo vijana watakuwa na mawazo thabiti inayoambatana na utekelezaji, basi wapo kwenye nafasi nzuri ya kutengeneza ajira kupitia uvumbuzi.
                KALU alitoa mifano ya vijana wenye umri mdogo katika nchi zilizo endelea ambao walifanikiwa kuanzisha makampuni makubwa duniani ambayo kwa sasa yanaajiri idadi kubwa ya watu. Katika hili, hakuwasahau wagunduzi wa Facebook  na Mozilla.
                Vijana waliuliza maswali mengi juu ya upatikanaji wa mitaji ili kujiajiri, hata hivyo ( KALU ) alisisitiza umuhimu  wa kuwa na mawazo thabiti” – VISION  inayotekelezeka kama msingi wa kujiajiri. Aliendelea kueza kuwa mafanikio madogo huandaa mazingira mazuri ya mafanikio makubwa hivyo akasisitiza umuhimu wa matumizi mazuri ya rasilimali kidogo tulizonazo katika kuandaa mazingira ya uwekezaji.
                Kongamano limeahilishwa, yapata saa kumi jioni………….
Kongamano hili kimedhaminiwa na TBC1, CLOUDS MEDIA, CREATIVE EYE, NMB, CRDB, MLIMANI TV AND AZANIA BANK.
                                Imeandaliwa na kuletwa kwenu na Konahabari.blogspot.com


No comments:

Post a Comment