Gender association na AMREF TANZANIA wamefanikiwa kutoa
semina juu ya mahusiano,Maambukizo ya virusi vya UKIMWI, Sheria zinazoongoza
mahusiano ya kijinsia, na nafasi ya kila mwanajamii katika kajali, kuheshimu na
kulinda utu na haki za Binadamu.
Semina hiyo imefanyika
leo tarehe 31/03/2012 Nyumba nambari b123 Kitivo Cha Biashara ( UDBS )
ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Chuo waliweza kuhudhuria.
Akiongea na idadi kubwa ya watu waliofika katika eneo hilo,
Profesa B. KODA kutoka ( IDS – UDSM )alitoa
ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayo wagusa Vijana katika maisha. Profesa
KODA alitisha mkazo kuhusu nafasi ya Vijana kujitambua, kuitambua thamani yao
na mchango wao katika jamii.
Wakisha kujitambua Vijana wanayo nafasi ya kujiepusha na
maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na kujihusisha katika mambo ya maendeleo. KODA
amewasihi Vijana kuwa waaminifu na kutopenda starehe za muda mfupi ambazo kwazo
maisha yao huharibika.
Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia KODA amezitaja sheria
zinazokataza kumlazimisha mtu katika mahusiano ya kimapenzi. Hii imetoa upeo
mpana zaidi kwa Vijana kuzijua sheria zinazoongoza mahusiano mema katika jamii.
No comments:
Post a Comment