Ikiwa ni sehemu ya agenda muhimu katika kujenga mitandao ya
kijamii na kiuchumi ( networking ), wanafunzi wa Kitivo Cha Biashara wa Chuo
Kikuu Dar es salaam walikutana katika ukumbi wa Mariot Hotel nje kidogo ya mji
wa Mabibo kujadili masuala ya msingi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kutathimini
suala la ukosefu wa ajira, fulsa za vijana kujiajiri na changamoto zilizopo
katika sector ya ajira.
Wakiwa katika ukumbi wa Mariot, Mameneja hao walipata nafasi
ya kujadili kwa kina umuhimu wa kuwekeza katika maarifa (elimu ) na Ushiriki katika mambo ya kijamii kwa lengo la kupata
uzoefu na fikra chanya ziletazo mabadiliko (networking).
Kwa mujibu wa LOTTU YONA, mdau mkubwa katika mkutano huo “Wazo /
idea” ni mtaji mkubwa katika utambuzi wa fulsa zilizopo ambazo kwazo vijana
wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali na kuongeza nafasi za ajira nchini.
KONAHABARI ilipata nafasi ya
pekee kuwatambua washiriki wengine kutoka Ujerumani, Kenya na Uganda ambao
walifurahishwa sana na juhudi za Wanafunzi wa UDSM katika masuala ya msingi ya
kitaifa.
ILIKUWA CKU NZURI SANA KWA FINALIST KWANI WATU WALIPATA ELIMU PAMOJA NA BURUDANI YA KUTOSHA MUCH RESPECT KWA BWANA CHAPPA(VENANCE) KWA KU COORDINATE MZIGO MZIMA
ReplyDelete