Somalia yaomba kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Somalia yaomba kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Somalia imetuma maombi ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
serikali ya Kenya ilitangaza katika waraka wake siku ya Jumanne (tarehe
6 Machi)."Maombi yamefuatia maendeleo makubwa nchini Somalia ambayo
yameonekana nchini kwa kuanza safari ya kujiimarisha na amani baada ya
miaka mingi ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe," rais wa Kenya, ambaye
ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, alisema katika waraka
wake.Maombi yatafikiriwa na nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Nchi
zilizounda soko la pamoja mwaka 2010 na zinashughulikia kuanzisha sarafu
ya pamoja mwaka huu.
No comments:
Post a Comment