Dar es salaam Stock of Exchange ( DSE ) imefanya kongamano
na wanafunzi –wahasibu (Accounting
Association of Dar es salaam University- AADU). Kongamano hilo limefanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Kitivo Cha Biashara Chuo Kikuu Dar es salaam
tarehe 24/03/2012.
Kongamano hilo limehudhuliwa na wadau mbalimbali wa mambo ya
kibiashara na wanafunzi kutoka idara na taasisi mbalimbali ndani na nje ya
Chuo. Kongamano lilifunguliwa mapema na katibu mkuu wa AADU Bwana Daynus Mgaya
ambaye aliwakalibisha wageni waliohudhuria katika kongamano hilo.
Mwakilishi wa DSE na
mtoa maada katika kongamano hilo Bwana
MOHAMED KAILWA alipata nafasi ya waelezea wahasibu na wadau wa mambo ya kibiashara, mambo
mbalimbali yahusuyo Dar es salaam Stock of Exchange ( DSE ) ikiwa ni pamoja na
njia mbalimbali za udhibiti na ukaguzi wa hesabu.
Bwana KAILWA alitoa maelezo yakinifu juu ya utaratibu wa
usajiri wa makampuni katika DSE ambapo alionesha kuongezeka kwa idadi ya
makampuni yanayosajiriwa kila mwaka, kwa mujibu wa KAILWA (DSE ) ilifanikiwa kusajiri makampuni 17
mwaka 2011 ikilinganishwa na idadi ya makampuni 15 yaliyo sajiriwa mwaka 2010
ambayo ni idadi sawa na makampuni 15 mwaka 2009.
Kailwa alitoa ufafanuzi juu ya fulsa zilizopo katika taaluma
ya Uhasibu na ukaguzi wa hesabu ( accounting and auditing ) kwamba wahasibu
wanayo fulsa nzuri ya kujiajiri katika sector ya ushauri wa mambo ya
kibiashara, udhibiti wa fedha, usimamizi wa miradi na ujasiliamali.
Mtoa maada huyo hakusita kuwatahadharisha wahasibu juu ya
hasara zitokanazo na udanganyifu katika ukaguzi wa hesabu ambapo, alisema
kwamba takwimu zisibitishwazo na wahasibu hutumiwa na taasisi nyingine katika
kutafuta fulsa za uwekezaji hivyo basi udhaifu wowote katika sector hii una
madhara kwa taifa, wawekezaji na taasisi za kibiashara.
KONAHABARI
ITAENDELEA KUWAJULISHA MATUKIO MBALIMBALI…………………….
KAILWA AKITOA SOMOKULIA NI OFISA MAHUSIANO WA DAR ES SALAAM MARKETING ASSOCIATION ( DUMA )
KATIKATI NI KATIBU MKUU WA AADU BWANA DAYNUS MGAYA
No comments:
Post a Comment