Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliueleza mkutano wa mwaka wa makamanda
na maofisa wa polisi kuheshimu haki za binadamu wakati wa utekelezaji
wa kazi zao, The Citizen la Tanzania liliripoti Jumanne (tarehe 6
Machi).Kikwete katika hotuba yake, alinukuu ripoti za matumizi makubwa
ya nguvu kwa watuhumiwa, na kueleza masikitiko kuhusu ongezeko la
malalamiko kutoka kwa wananchi. “Ninataka mlijadili hili na kutafuta
njia za kulimaliza,” Kikwete alisema Jumatatu. “Ikiwa ni pamoja na suala
la nidhamu katika mitaala ya vyuo vya mafunzo ya polisi,” aliongeza.
Kauli ya Kikwete ilikuja wakati idadi ya maofisa wa polisi
waliripotiwa kwa kutuhumiwa kwa utovu wa nidhamu. Kikwete alitumia mfano
wa ofisa wa polisi huko Moshi ambaye alitiwa mbaroni kwa kuacha kituo
chake, akikutwa katika ukumbi wa disko akiwa na bombomu yenye risasi.
No comments:
Post a Comment