Mark Zuckerberg ( kushoto )
- Ni Myahudi mkazi wa Marekani
- Kijana mdogo aliyepata mafanikio makubwa na ulimwengu kumtambua kuwa bilionea mwenye mdogo kuliko wote duniani
MTANDAO
wa Facebook uligunduliwa na mwanafunzi wa masomo ya sayansi wa Chuo
Kikuu cha Harvard, Mark Zuckerberg, akishirikiana na wanafunzi wenzake,
Eduardo Saverin, Dustin Moskovitz na Chris Hughes.
Alitumia
maarifa yake ya sayansi ya kompyuta vizuri kwa kuingia katika mtandao
wa usalama wa Chuo Kikuu cha Harvard na kunakili picha kutoka kwenye
vitambulisho vya wanafunzi wenzake vilivyokuwa vikitumiwa katika mabweni
ili kuuboresha mtandao wake wa Facemash.
Mtandao
wa Facemash ulianza kufanya kazi Oktoba 28, 2003, na ulifungwa siku
chache baadaye na uongozi wa Harvard kuupiga marufuku.
Zuckerberg
alifunguliwa mashitaka ya kukiuka masuala ya usalama, kukiuka
hakimiliki na kukiuka uhuru wa mtu binafsi, kwa kuiba picha za wanafunzi
wenzake alizotumia kuutangaza mtandao wake. Hata hivyo mashitaka yote baadaye yalitupiliwa mbali.
Februari 4, 2004, Zuckerberg alizindua upya mtandao wake na kuupa jina la ‘TheFacebook’.
Siku
sita baadaye, Zuckerberg tena aliingia matatani wakati wanafunzi
wenzake wa Harvard; Cameron Winklevoss, Tyler Winklevoss na Divya
Narendra, walipomtuhumu kuwaibia mawazo yao ya kudhamiria kuanzisha
mtandao wa kijamii wenye jina la HarvardConnection, pia kwa kutumia
ubunifu wao kutengeneza mtandao wa TheFacebook.
Winklevoss,
Winklevoss na Narendra baadaye walimfungulia mashitaka Zuckerberg. Hata
hivyo shauri hilo pia lilimalizwa nje ya mahakama.
Uanachama
wa mtandao huo awali ulizuiliwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Harvard lakini Zuckerberg aliwaandikisha baadhi ya wanafunzi
wenzake ili kusaidia kuukuza mtandao wake: Eduardo Saverin
alishughulikia mambo ya biashara, Dustin Moskovitz kama ‘programmer’,
Andrew McCollum kama ‘graphic artist’ na Chris Hughes. Kwa pamoja timu
hiyo iliupanua mtandao huo hadi katika vyuo vikuu na vyuo vingine vya
kawaida.
Mwaka 2004, mwekezaji, Sean Parker (mwanzilishi wa Napster) alifanywa kuwa rais wa kampuni.
Kampuni ilibadilisha jina kutoka TheFacebook kuwa Facebook,baada ya kununua umiliki wa jina facebook.com mwaka 2005 kwa dola 200,000.
Baadaye
Zuckerberg alitambulika kuwa bilionea (mdogo kwa umri) kuliko wote duniani.
hakika, mafanikio hayaangalii umri bali uwezo wa mtu kuzifikilia fulsa na kuzitumia pasipo kujali changamoto ziambatanazo na mafanikio yatarajiwayo. Huu ni ujumbe kwa watu wenye malengo na fikra za ujasiliamali duniani.
I LIKE THIS POST
ReplyDeletedah!,jamaaa ni kichwa!,akili zake zimemwezesha kuwa bilionea.ni jambo kubwa mno.tunapaswa kuiga mfano wake
ReplyDelete