Rais mstaafu- Benjamini W. Mkapa amehudhuria katika Kigoda
Cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu Dar es salaam. Kigoda cha Mwalimu Nyerere mwaka
2012 ni mwendelezo wa makongamano makumbwa ambayo hufanyika kila mwaka katika
Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es salaam. Endelea……
Profesa Mukandala akifungua kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere
Makongamano haya hubeba hisia na maada mbalimbali zinazo
tukumbusha harakati na za ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya ukoloni unaochukua
sura tofauti katika awamu mbalimbali. Hii ni sehemu pekee ambayo Washiriki
hupata nafasi ya kujikumbusha harakati za Mwalimu Nyerere katika kuujenga umoja
wa kitaifa na mchango wake kiujumla kwa
bara la Afrika.
Hisia na maoni ya wanamapinduzi wengine katika kumkomboa
mwafrika hubainishwa. Marcus Garvery Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika na
Mpigania haki za watu weusi Duniani aliwahi kusema “ sitambui uwepo wa mipaka
ambapo mtu mweusi yupo, Ulimwengu wote ni jimbo langu mpaka Mtu mweusi awe
huru”
Tofauti na makongamano mengine, Kongamano la mwaka huu
limebebwa na maada kuu isemayo “TAFAKURI JUU YA WASANII KATIKA UKOMBOZI”.
Wazungumzaji wakuu katika kongamano hilo ni pamoja na Micere Mugo, Abdillatif
Abdalla na Professa Isa Shifji- Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Dar es salaam.
Micere Mugo alipata nafasi ya kuelezea kwa ufasaha nafasi ya
Sanaa na Wasanii katika harakati za ukombozi wa Mwafrika. Micere amekipongeza Chuo Kikuu Cha Dar es
salaam kuwa sehemu muhimu katika kukumbuka harakati na mchango wa watu
mbalimbali katika ukombozi wa Mwafrika. Ameizungumzia sanaa kama sehemu muhimu
katika kuukuza utamaduni wa Mwafrika. Micere alibainisha kuwa kukuza Kiswahili
ni sehemu ya ushindi katika Ukombozi wa
kifikra wa mtu mweusi.
Kwa upande wake Abdillatif Abdalla ameweka wazi mambo
mbalimbali na zaidi nafasi ya Wasanii katika ujenzi wa utamaduni wa Mwafrika.
Historia ya Ukombozi wa Mtu mweusi haujawahi kuiacha sanaa kama silaha muhimu
ya ukombozi.
Profesa Shifji kwa
upande wake ameufananisha utamaduni na Utu, Uzalendo na Roho ya Taifa. Pasipo kujali Utamaduni wetu ni sawa na kuupuuza
Utu wetu na kukosa Uzalendo kwa Taifa letu. Hakusita pia kusisitiza mchango wa
Mwalimu Nyerere juu ya ujenzi wa Taifa huru lenye maadili na misingi bora
Katika utamaduni wake.
Kongamano linaendelea katika ukumbi wa Nkurumah Kesho tarehe
13/04/2012……
Konahabari imefanikiwa kupiga picha katika ukumbi wa Nkuruma
leo…….
Pamoja tulijenge taifa letu- imerekodiwa na konahabari.blogspot.com
picha nyingine......
Washiriki wa Kigoda Cha Mwalimu wakipata Vitabu.nje ya Ukumbi wa Nkurumah....Muimbaji katika Kigoda Cha Mwalim Nyerere......
Profesa Issa Shivji akitoa somo Nkurumah hall
Washiriki toka nchi mbalimbali katika Ukumbi wa Nkurumah......
endelea kutembelea Konahabari, kwa maoni / ushauri click kichwa cha post upate maelezo ya kutuma hisia zako....
imetulia hiyo
ReplyDelete