Msafiri Mbwambo miaka 32 ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya
Usa-River, wilayani Arumeru mkoani Arusha, ameuawa
kinyama kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.
Tukio hili limetokea wakati nchi ipo katika wakati mgugu wa kutafakari hatma ya umasikini wa walio wengi na umuhimu wa kupunguza (gap) kati ya walionacho na wasionacho. Umuhimu wa kupata Viongozi Bora watakao tunga sheria zinazo weza kudhibiti mianya ya Rushwa na Ubadhilifu wa mali za umma kwa maslahi ya kizazi kilichopo na kijacho.
Mbwambo
aliuawa na watu wasiojulikana baada ya kupigiwa simu kumwita majira ya
saa mbili usiku, wakati akitazama taarifa ya habari eneo la Mji Mwema
akiwa na watu wengine.
Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Arumeru, Dotnan
Ndonde, alisema mara baada ya marehemu kuondoka muda mfupi baadaye,
mwili wake uliokotwa eneo la Shule ya Mukidoma, Kusini mwa mji wa
Usa-River umbali wa takriban kilomita mbili kutoka alipokuwa.
“Tulimkuta
akiwa anavuja damu ilionekana muda si mrefu alikuwa amechinjwa na watu
wasiojulikana ambao walikuwa wametoweka,”alisema Ndonde
Wapenzi na Wanachama wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA-Chuo Kikuu Dar es salaam) wamelaani kitendo hicho na kudai kuwa kitendo hicho ni kinyume kabisa na haki za binadamu.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawa kusita kotoa hisia zao kuhusiana na tukion hilo la kinyama Arusha.
Ndonde alisema kwa mazingira ya tukio na hali ya kisiasa eneo la Meru, anashindwa kuyatenganisha mauaji hayo na siasa.
Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) Bwana Joshua Nassari ameeleza
kusikitishwa kwake na tukio hilo la kinyama na kusema kuwa bado joto la
kisiasa lipo juu wilayani humo na zaidi amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha
linawasaka na kuwashughulikia ipasavyo wale wote waliohusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment