Rais wa Malawi Bingu wa amefariki dunia baada ya
kupatwa na mshtuko wa moyo, akiwa na miaka 78. Mwili wa wa kiongozi huyo umepelekwa
Afrika Kusini. Hata hivyo serikali haijatoa taarifa rasmi kuhusu kifo
chake.Wa-Mutharika alikufa baada ya moyo wake kusimama.
Wadadisi wa mambo wamesema kuwa kifo cha rais huyo huenda
kikazua mgogoro wa uwongozi nchini Malawi. Katiba ya nchi inampa nafasi Makamu wa Rais
kuongoza nchi endapo Rais atafariki au kuugua kiasi cha kushindwa
kuongoza taifa.Hata hivyo Makamu wa Rais nchini Malawi, Joyce Banda
alitofautiana na Wa-Mutharika kufuatia mzozo wa urithi wa uongozi ambapo
alifukuzwa kutoka chama tawala,Democratic People's Party (DPP).Kakake rais ambaye ni Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika aliteuliwa kugombea urais hapo mwaka wa 2014. Maiti ya Rais imesafirishwa Afrika Kusini huku maafisa wakitafakari hali ya sasa.
Bingu wa Mutharika aliingia madarakani mwaka wa 2004. Baadaye alikihama chama chake cha United Democratic Front (UDF) kwa tuhuma za wanachama kuhujumu harakati za kupambana na ufisadi. Alichaguliwa tena mwaka 2009, lakini katika siku za karibuni wakosoaji wake wamemlaumu kwa kuegemea sera za kiimla.
Rais huyo alikumbwa na shinikizo za kuachia madaraka kwa tuhuma za kupendelea ukoo wake, na kuharibu madaraka.Wa Mutharika aliwakera wafadhili wa kigeni hasa baada ya kumfukuza balozi wa Uingereza nchini Malawi.
No comments:
Post a Comment