Saturday, March 31, 2012

DAR ES SALAAM UNIVERSITY ENTREPRENEURSHIP FORUM (DUEF) YAFUNGUA FIKRA CHANYA ZA VIJANA KUJIAJIRI


DUEF imefanya kongamano kubwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es salaam, Wajasiliamali na Waandishi wa habari. Kongamano hilo limefanyika leo tarehe 31/03/2012 katika nyumba namba b126 jengo jipya la Kitivo Cha Biashara Chuo Kikuu Dar es salaam.
        Maada kuu katika kongamano hilo ni “Ujasiliamali kwa Maendeleo ya Vijana”
       Akiongea na jopo la wanazuoni waliohudhuria katika kongamano hilo Miss ELIZABETH ( mtoa maada katika kongamano hilo) aliwasihi vijana kujiamini na kubuni miradi mbalimbali itakayowawezesha kujiajiri.
         Kwa upande wake aliwashauri Vijana kujiunga na Biashara ya mtandao inayofahamika kama Network Marketing ambayo kwa mujibu wa Elizabeth, biashara hii imekuwa chanzo cha mafanikio ya mabilionea wengi duniani.
ELIZABETH pia hakusita kuwasihi vijana kutumia fursa zilizopo katika kujenga misingi bora ya maisha yao badala ya kusubiri fulsa zitakazopatikana watakapomaliza masomo yao. Akimtumia MICHAEL DELL kama mfano wa kuigwa ( Mmiliki wa kampuni kubwa ya utengenezaji wa Komputer ambaye alifungua kampuni yake akiwa masomoni ). ELIZA alisema inawezekana kwa yeyote aliye na “VISION”
Mtoa maada mwingine katika kongamano hilo ni JOFREY TENGANAMBA – Mhitimu wa Chuo Kikuu Dar es salaam aliyepata umaarufu mkubwa katika tasnia ya utunzi wa Vitabu kikiwemo kitabu cha “KICHWA CHANGU NI HAZINA YA UTAJIRI”.  TENGANAMBA alisisitiza zaidi suala la Vijana kujiamini ili kufikia malengo.
Kushoto ni Miss ELIZABETH akitoa somo

  Imerekodiwa na kuletwa kwako na konahabari- Blog ya kwanza kuifikia hisia yako……

 

GENDER NA AMREF TANZANIA WATOA SEMINA UDSM


Gender association na AMREF TANZANIA wamefanikiwa kutoa semina juu ya mahusiano,Maambukizo ya virusi vya UKIMWI, Sheria zinazoongoza mahusiano ya kijinsia, na nafasi ya kila mwanajamii katika kajali, kuheshimu na kulinda utu na haki za Binadamu.
Semina hiyo imefanyika  leo tarehe 31/03/2012 Nyumba nambari b123 Kitivo Cha Biashara ( UDBS ) ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Chuo waliweza kuhudhuria.
Akiongea na idadi kubwa ya watu waliofika katika eneo hilo, Profesa B. KODA  kutoka ( IDS – UDSM )alitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayo wagusa Vijana katika maisha. Profesa KODA alitisha mkazo kuhusu nafasi ya Vijana kujitambua, kuitambua thamani yao na mchango wao katika jamii.
Wakisha kujitambua Vijana wanayo nafasi ya kujiepusha na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na kujihusisha katika mambo ya maendeleo. KODA amewasihi Vijana kuwa waaminifu na kutopenda starehe za muda mfupi ambazo kwazo maisha yao huharibika.
Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia KODA amezitaja sheria zinazokataza kumlazimisha mtu katika mahusiano ya kimapenzi. Hii imetoa upeo mpana zaidi kwa Vijana kuzijua sheria zinazoongoza mahusiano mema katika jamii.
                Imerekadiwa na kuletwa kwako na konahabari( blog ya kwanza kuzifikia hisia zako)
Profesa KODA akitoa semina kwa wanafunzi


Friday, March 30, 2012

ARSENAL WENGER AFUNGIWA MECHI TATU NA UEFA





Meneja wa Arsenal , Arsene Wenger wa amefungiwa mechi tatu za UEFA na kutozwa faini ya 40 000 ($ 53 100) kwa sababu ya kujibizana na maafisa wa mechi baada ya kutolewa katika ligi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya AC Milan mwezi huu.

UEFA ilisema Ijumaa kuwa Mfaransa huyo alipatikana na hatia ya mwenendo mbaya katika mzunguko wa pili wa raundi ya 16 ambayo Arsenal ilishinda 3-0 na kutolewa nje kwa jumla ya mabao 4-3.

" Arsene Wenger  amesimamishwa mechi tatu  za mashindano yajayo ya UEFA na badala yake Kocha msaidizi ndiye atakaye simamia timu katika mechi zote tatu


TAARIFA YA MSIBA KUTOKA KATIKA FAMILIA YA NDUGU SHIRIMA


Familia ya Ndugu Shirima wa Moshi wakiaga mwili wa mpendwa wao  Francis Shirima.
Marehemu Francis Shirima ni Baba mzazi wa Beatrice ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitivo cha Biashara Chuo Kikuu Dar es salaam. Safari ya kumuaga marehemu Francis Shirima ilianza mida ya saa sita mchana ambapo wanafunzi wa Kitivo Cha Biashara walioonekana kuwa na nyuso za huzuni walianza kujikusanya katika eneo la Kontena tayari kwa safari ya kwenda kanisani.
Misa ya kumuaga marehemu Francis ilifanyika kwa mujibu wa taratibu za kanisa zilizopewa kibali mbele za Mungu kwa ajiri ya sifa na utukufu wake.
Msemaji wa familia kwa niaba ya familia, ndugu na jamaa alitoa shukrani za dhati kwa Watu, taasisi na jumuiya mbalimbali zilizo husika kwa namna moja au nyingine kushirikina nao katika msiba huo.
Msemaji alipata nafasi ya kutoa historia fupi ya Marehemu ambapo alisema “Marehemu Francis Shirima alizaliwa mwaka 1956 katika wilaya ya Moshi – Mkoani Kilimanjaro. Alijipatia Elimu yake katika Shule mbalimbali kabla ya kuanza kujihusisha na shughuli za kilimo na Biashara.
Marehemu alikuwa akipata matibabu katika Hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo Hospital ya Agakani  na Hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Moshi kwa Mazishi, Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi….!
            Imerekodiwa na Konahabari…..
 Watu wakiingia kanisani 

 msemaji wa familia ya Shirima akitoa historia fupi ya marehemu
 watu wakitoka kanisani baada ya misa ya kumuaga marehemu

 mwili wa marehemu unaingizwa kwenye gari

 Watu wakiangalia msafara wa gari zilizoondoka kumsindikiza marehemu

Monday, March 26, 2012

MWANAMKE AKIMBIA BAADA YA KUSABABISHA AJALI


Mwanamke mmoja alifanikiwa kukimbia baada ya kusababisha ajali ya gari katika eneo la Mabibo Stand siku ya tarehe 24/03/2012 saa tano usiku. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, Mwanamke huyo alionekana kuteteleka na kuyumba kabla ya gari yake aliyokuwa akiiendesha kuacha njia na kuingia katika mfereji eneo la Mabibo Hostel - bara bara inayounganisha eneo la Ubungo na Buguruni ( Mandela road )
               Watu wengi walikusanyika katika eneo hilo kushuhudia kilichotokea lakini hadi kufikia saa sita kamili usiku Mama huyo hakuweza kurudi katika eneo la tukio na hivyo kuwalazimu Polisi kuliondoa Gari hilo katika eneo la tukio saa tisa na dakika kumi na tatu usiku.
                Konahabari   ilifanikiwa kupata picha ifuatayo katika eneo hilo lililotawaliwa na amsha amsha za hapa na pale zikizoonesha mvutano wa kimaslahi kama sio kiuwajibikaji…………….

Sunday, March 25, 2012

MAMENEJA UDSM WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA AJIRA NCHINI.

Ikiwa ni sehemu ya agenda muhimu katika kujenga mitandao ya kijamii na kiuchumi ( networking ), wanafunzi wa Kitivo Cha Biashara wa Chuo Kikuu Dar es salaam walikutana katika ukumbi wa Mariot Hotel nje kidogo ya mji wa Mabibo kujadili masuala ya msingi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kutathimini suala la ukosefu wa ajira, fulsa za vijana kujiajiri na changamoto zilizopo katika sector ya ajira.
Wakiwa katika ukumbi wa Mariot, Mameneja hao walipata nafasi ya kujadili kwa kina umuhimu wa kuwekeza katika maarifa (elimu ) na Ushiriki katika mambo ya kijamii kwa lengo la kupata uzoefu na fikra chanya ziletazo mabadiliko (networking).
 Kwa mujibu wa LOTTU  YONA, mdau mkubwa katika mkutano huo “Wazo / idea” ni mtaji mkubwa katika utambuzi wa fulsa zilizopo ambazo kwazo vijana wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali na kuongeza nafasi za ajira nchini.
                KONAHABARI ilipata nafasi ya pekee kuwatambua washiriki wengine kutoka Ujerumani, Kenya na Uganda ambao walifurahishwa sana na juhudi za Wanafunzi wa UDSM katika masuala ya msingi ya kitaifa.













Saturday, March 24, 2012

WAHASIBU UDSM WAFANYA KWELI UDBS


Dar es salaam Stock of Exchange ( DSE ) imefanya kongamano na wanafunzi –wahasibu  (Accounting Association of Dar es salaam University- AADU). Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kitivo Cha Biashara Chuo Kikuu Dar es salaam tarehe 24/03/2012.
Kongamano hilo limehudhuliwa na wadau mbalimbali wa mambo ya kibiashara na wanafunzi kutoka idara na taasisi mbalimbali ndani na nje ya Chuo. Kongamano lilifunguliwa mapema na katibu mkuu wa AADU Bwana Daynus Mgaya ambaye aliwakalibisha wageni waliohudhuria katika kongamano hilo.
Mwakilishi  wa DSE na mtoa maada  katika kongamano hilo Bwana MOHAMED KAILWA alipata nafasi ya waelezea wahasibu  na wadau wa mambo ya kibiashara, mambo mbalimbali yahusuyo Dar es salaam Stock of Exchange ( DSE ) ikiwa ni pamoja na njia mbalimbali za udhibiti na ukaguzi wa hesabu.
Bwana KAILWA alitoa maelezo yakinifu juu ya utaratibu wa usajiri wa makampuni katika DSE ambapo alionesha kuongezeka kwa idadi ya makampuni yanayosajiriwa kila mwaka, kwa mujibu wa KAILWA  (DSE ) ilifanikiwa kusajiri makampuni 17 mwaka 2011 ikilinganishwa na idadi ya makampuni 15 yaliyo sajiriwa mwaka 2010 ambayo ni idadi sawa na makampuni 15 mwaka 2009.
Kailwa alitoa ufafanuzi juu ya fulsa zilizopo katika taaluma ya Uhasibu na ukaguzi wa hesabu ( accounting and auditing ) kwamba wahasibu wanayo fulsa nzuri ya kujiajiri katika sector ya ushauri wa mambo ya kibiashara, udhibiti wa fedha, usimamizi wa miradi na ujasiliamali.
Mtoa maada huyo hakusita kuwatahadharisha wahasibu juu ya hasara zitokanazo na udanganyifu katika ukaguzi wa hesabu ambapo, alisema kwamba takwimu zisibitishwazo na wahasibu hutumiwa na taasisi nyingine katika kutafuta fulsa za uwekezaji hivyo basi udhaifu wowote katika sector hii una madhara kwa taifa, wawekezaji na taasisi za kibiashara.
                KONAHABARI ITAENDELEA KUWAJULISHA MATUKIO MBALIMBALI…………………….
 KAILWA AKITOA SOMO


 KULIA NI OFISA MAHUSIANO WA DAR ES SALAAM MARKETING ASSOCIATION ( DUMA )




 KATIKATI NI KATIBU MKUU WA AADU BWANA DAYNUS MGAYA

Friday, March 23, 2012

OFISA MAHUSIANO ( DUMA ) AZALIWA…….


Hizi ni picha zilizopigwa usiku wa tarehe 22/03/2012 katika Ukumbi wa London, nje kidogo ya Mabibo Hostel ambapo jopo la wanazuoni kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam walikutana kumpongeza Ofisa Mahusiano wa Dar es salaam University Marketing Association ( DUMA ) Bwana Enock Ngulwa  ambaye alikuwa anasherehekea siku yake ya Kuzaliwa.
Bwana Ngulwa aliyejipatia umaarufu mkubwa katika ushawishi na uongozi ndani ya DUMA na taasisi mbalimbali za Kibiashara nchini, alifurahishwa sana na ujio wa wanazuoni hao ambapo alisisitiza umoja na mshikamano wa kijamii katika kufikia malengo. Zaidi ya yote alimshukuru Mungu kwa namna ya pekee ambaye amekuwa msaada mkubwa katika mafanikio yake.

KONAHABARI inamtakia maisha mema na yenye Baraka………