Monday, April 2, 2012

CHADEMA YASHINDA UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI

MGOMBEA wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari ameshinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana tarehe 01/04/2012

Msimamizi wa uchaguzi huo, Trasence Kagenzi, amemtangaza Nassari kuwa mshindi kwa kupata kura 32,672, na kumshinda mpinzani wake mkubwa, Sioi Sumari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura, 26,757. 

Matokeo ya awali jana, yalionesha kuwa  mgombea wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) Bwana Joshua Nasari alikuwa akiongoza katika vituo vya mjini wakati mwenzake Sioi alikuwa anafanya vizuri maeneo ya Vijijini.
         Konahabari ilifanikiwa kukuletea mfululizo wa matokeo katika vituo mbalimbali kama ilivyooneshwa katika page zilizotangulia zinazoonesha jinsi CHADEMA ilivyokuwa inakikiacha CCM kwa idadi kubwa ya kura katika Vituo mbalimbali.
        Mungu awabariki wana Arumeru, Mungu aibariki Tanzania........

No comments:

Post a Comment