Tuesday, April 24, 2012

CHELSEA WAMLIZA TENA BACELONA


Hatimaye Chelsea wafanikiwa kuiondoa Bacelona katika michuano ya kuwania Kombe la UEFA mwaka huu baada ya kulazimisha sare ya kufungana Bao mbili kwa mbili katika uwanja wa Nou Camp- ngome kuu ya Bacelona. Mechi hiyo imemalizika dakika chache zilizopita ambapo ulimwengu umeshuhudia mabingwa hao wa soka duniani wakiondoka uwanjani mikono nyuma.
Bacelona walikuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za Chelsea mapema kabisa katika dakika 45 za kipindi cha kwanza. Hawakuwa muda mrefu sana Bacelona kuongeza bao la pili lililoamsha hisia za ushindi miongoni mwa wachezaji wa Chelsea.
Dakika moja tu ya nyongeza baada ya 45 za kwanza kumalizika ilitosha kuwaamsha washabiki wa Chelsea vitini baada ya timu yao kujipatia bao la kwanza. Kindumbwendumbwe cha kusaka ubingwa kiliendelea kwa dakika 45 za kipindi cha pili ambapo Bacelona waliliandama lango la Chelsea kwa chenga na pasi nyingi zisizo na idadi. Chelsea kwa upande wao waliendelea kulinda lango lao huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza katika lango la Bacelona. 
Baada ya dakika 90 za mchezo, dakika ya kwanza ya nyongeza ilirudisha kilio Bacelona baada Chelsea kujipatia bao la pili.

No comments:

Post a Comment