Monday, April 23, 2012

TIMU YA UDBS YATUNISHIANA MISULI NA TIMU YA ARDHI UNIVERSITY.

 KIKOSI CHA UDBS KILICHOKABILIANA NA WACHEZAJI WA ARDHI.
Wanafunzi wa kitivo cha biashara Chuo kikuu Dar es salaam ( UDBS ) walicheza mchezo wa kirafiki ( mpira wa miguu ) katika uwanja wa michezo Chuo Kikuu Ardhi mwishoni mwa juma hii. 
Mechi hiyo ilikuwa na amsha amsha, ari kubwa ya mchezo na hasama miongoni mwa wachezaji na washabiki wa timu zote mbili. 
Timu zote zilishambuliana kwa awamu huku kila moja ikijaribu kuchukua ushindi wa kishindo katika mechi. Hata hivyo, mpaka mwisho wa mchezo Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana goli mbili kwa mbili.
        imeandaliwa na kuletwa kwenu na mwandishi wa konahabari Chuo Kikuu Ardhi.

No comments:

Post a Comment