Wednesday, April 18, 2012

REAL MADRID HOI - MBELE YA BAYERN MUNICH

 
Mambo hayakuwa mambo jana kwa wapenzi na mashabiki wa  Real Madrid pale timu yao iliposhidwa kufulukuta dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa Ulaya. Hii ni baada ya kukubali kipigo cha bao mbili kwa moja.                 
Mshambulizi Franck Ribery alikuwa wa kwanza kuliona lango la Real Madrid pale alipofumua mkwaju mkali na kumuacha kipa Iker Casillas akicheka na nyasi.                      
           Dakika saba tu baada ya kipindi cha pili kuanza zilitosha kuwanyanyua Mashabiki wa Madrid kote duniani baada ya  Mesut Ozil kuipatia Madrid bao zuri la kusawazisha. 
Maisha ya dakika tisini kama karne yaliendelea kutafsiriwa tofauti miongoni mwa wapenzi wa kandanda duniani hususani mashabiki wa Madrid na Bayern. 
            Kitendawili kiliteguka dakika chache kabla ya mpira kuisha pale ambapo Gomez aliwanyanyua tena mashabiki wa Bayern na kufunga hesabu ya mabao katika mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment