Tuesday, April 3, 2012

POLISI WAWADHIBITI MACHINGA UBUNGO

jeshi la Polisi limefanikiwa kuyadhibiti maeneo ya Ubungo Songas baada ya kuwafukuza wafanyabiashara wadogo wadogo wajulikanao kwa jina la Machinga. Tukio hilo limetokea leo tarehe 03/04/2012 ambapo Polisi la kutuliza ghasia ( FFU ) walionekana kulinda eneo la Ubungo Songas baada ya kuwafukuza wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.
Konahabari ilifanikiwa kuongea na baadhi ya wafanya biashara wa eneo hilo kutaka kujua chanzo cha tukio hilo. Mmoja wa Wafanyabiashara hao alieleza kuwa sababu ya kuondolewa ni kwamb, maeneo hayo yanapakana na mitambo ya Ges ya Songas ambayo yanaweka kuleta madhara makubwa kwa wafanyabiashara hao na watu wengine katika eneo hilo endapo yakilipuka.
Hata hivyo mfanyabiashara huyo hakusita kueleza kuwa hakurizishwa na utaratibu wa kuwatoa katika eneo hilo na hivyo kuahidi kurudi katika eneo hilo pindi Polisi watakapo ondoka.
 picha iliyovutwa na kamera zetu ikionesha Polisi wakipiga doria.
 Watu wachache wakiwa katika eneo la Ubungo Songas baada ya Polisi kuwafukuza Machinga.

No comments:

Post a Comment