Monday, April 9, 2012

WASIFU PEKEE WA STEVEN KANUMBA


Wasifu wa Marehemu Steve Kanumba unazidi uwezo wa fikra za watu wengi kuweza kuuelezea. watu wengi wameweza kuongea kwa hisia tofauti namna walivyo mfahamu marehemu Kanumba. Hata hivyo, wengi wao hawajafanikiwa kuuelezea uhalisia wa kijana huyu wa pekee wa kitanzania katika karne ya 21. 
Sio rahisi sana kuzijua falsafa za Kanumba na hasa kwa mtu ambaye anaifikiria zaidi sehemu ya fani ya marehemu Kanumba kuliko maudhui katika filamu zake. Kanumba alifanikiwa sana katika kazi zake kwa kuwa aliweza kuutumia uwezo wake wa kufikilia kuziunganisha fikra za makundi mbalimbali ya kijamii. Aliweza kuigiza kama mtu wa aina yeyote awe tajiri au masikini wa mjini au kijijini. Kanumba alikuwa na ujasiri wa ajabu katika uigizaji kwa mfano, mazingira ya kutisha ya nguvu za giza kama vile Moses na filamu nyingine nyingi alizo washirikisha wasanii maarufu nchini. Hii ingekuwa tofauti sana kwa baadhi ya waigizaji duniani ambao wangezifikiria nafsi zao kabla ya kukubali kuigiza katika maeneo fulani ya kutisha au yanayoonekana kudharirisha au kuutia mwili unyonge wa kifikra au kimwili. Hakika pengo la Kanumba halitazibika Historia yatukumbusha mengi juu ya Marehemu Kanumba ambayo jamii itayakumbuka daima. Ni nani ataigiza kama Kanumba katika Johari part 2 ? Ni nani ataigiza kama Kanumba katika RIZIKI ? Ni nani atabeba hisia kama Kanumba katika Dangerous Dasire ? maswali haya hayana majibu mepesi bali kumuachia Mungu ambaye ndiye muumba wa vyote. Mungu ailaze roho ya marehemu Kanumba mahala pema peponi.

No comments:

Post a Comment