Friday, April 13, 2012

NANI AUNDE SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA ARDHI ?


Harakati za Uchaguzi wa serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Cha Ardhi zimeanza. Wakiongea na Konahabari jana, Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu -ARDHI waliokuwa  katika kampeni za awali za kumnadi mgombea wao Mr. Chacha walieleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kupata viongozi imara katika ngazi za Vyuo Vikuu ili kuandaa taifa bora siku za usoni.
Wasomi ndio viongozi wa taifa, watu wenye dira halisi na mtazamo yakinifu juu ya kizazi kilichopo na kijacho. Wao ndio wenye jukumu kubwa katika kutambua na kuchagua mifumo bora ya uongozi ambayo kwayo haki za binadamu zitalindwa na ustawi wa jamii utaboreshwa.
"Kushindwa kuchagua viongozi bora na wenye mtazamo chanya katika ustawi wa jamii ni kuchagua mwelekeo mbaya wa Vyuo vyetu" ,alisema mwanafunzi wa ARDHI UNIVERSITY.  
Mr. Chacha ambaye ni mgombea wa nafasi ya Urais - serikali ya wanafunzi ameahidi kuwatumikia wanafunzi wa Chuo hicho na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Ushirikiano katika uongozi ni silaha muhimu ya kufikia malengo, alisema Bwana Chacha.
                               Endelea kuitembelea konahabari  upate kujua mengi zaidi………. 
 Mr. Chacha akipeana mkono na meneja kampeni katika eneo la seven ways Chuo Kikuu Cha ARDHI
Wanafunzi wa Chuo Cha ARDHI wakimsikiliza mgombea.

No comments:

Post a Comment