Thursday, April 12, 2012

MKAPA NDANI YA KIGODA CHA NYERERE UKUMBI WA NKURUMAH –UDSM


Rais mstaafu- Benjamini W. Mkapa amehudhuria katika Kigoda Cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu Dar es salaam. Kigoda cha Mwalimu Nyerere mwaka 2012 ni mwendelezo wa makongamano makumbwa ambayo hufanyika kila mwaka katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Dar es salaam. Endelea……
Mkapa akisalimiana na Abdilatit Abdalla
 Profesa Mukandala akifungua kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere
             
Makongamano haya hubeba hisia na maada mbalimbali zinazo tukumbusha harakati na za ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya ukoloni unaochukua sura tofauti katika awamu mbalimbali. Hii ni sehemu pekee ambayo Washiriki hupata nafasi ya kujikumbusha harakati za Mwalimu Nyerere katika kuujenga umoja wa kitaifa na mchango wake  kiujumla kwa bara la Afrika.
Hisia na maoni ya wanamapinduzi wengine katika kumkomboa mwafrika hubainishwa. Marcus Garvery Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika na Mpigania haki za watu weusi Duniani aliwahi kusema “ sitambui uwepo wa mipaka ambapo mtu mweusi yupo, Ulimwengu wote ni jimbo langu mpaka Mtu mweusi awe huru”
Tofauti na makongamano mengine, Kongamano la mwaka huu limebebwa na maada kuu isemayo “TAFAKURI JUU YA WASANII KATIKA UKOMBOZI”. Wazungumzaji wakuu katika kongamano hilo ni pamoja na Micere Mugo, Abdillatif Abdalla na  Professa Isa Shifji- Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es salaam.
Micere Mugo alipata nafasi ya kuelezea kwa ufasaha nafasi ya Sanaa na Wasanii katika harakati za ukombozi wa Mwafrika.  Micere amekipongeza Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuwa sehemu muhimu katika kukumbuka harakati na mchango wa watu mbalimbali katika ukombozi wa Mwafrika. Ameizungumzia sanaa kama sehemu muhimu katika kuukuza utamaduni wa Mwafrika. Micere alibainisha kuwa kukuza Kiswahili ni sehemu ya ushindi katika Ukombozi wa  kifikra wa mtu mweusi.
Kwa upande wake Abdillatif Abdalla ameweka wazi mambo mbalimbali na zaidi nafasi ya Wasanii katika ujenzi wa utamaduni wa Mwafrika. Historia ya Ukombozi wa Mtu mweusi haujawahi kuiacha sanaa kama silaha muhimu ya ukombozi.
 Profesa Shifji kwa upande wake ameufananisha utamaduni na Utu, Uzalendo na Roho ya Taifa.  Pasipo kujali Utamaduni wetu ni sawa na kuupuuza Utu wetu na kukosa Uzalendo kwa Taifa letu. Hakusita pia kusisitiza mchango wa Mwalimu Nyerere juu ya ujenzi wa Taifa huru lenye maadili na misingi bora Katika utamaduni wake.
Kongamano linaendelea katika ukumbi wa Nkurumah Kesho tarehe 13/04/2012……
Konahabari imefanikiwa kupiga picha katika ukumbi wa Nkuruma leo…….
Pamoja tulijenge taifa letu- imerekodiwa na konahabari.blogspot.com
           picha nyingine......
 Washiriki wa Kigoda Cha Mwalimu wakipata Vitabu.nje ya Ukumbi wa Nkurumah....
 Muimbaji katika Kigoda Cha Mwalim Nyerere......
Profesa Issa Shivji akitoa somo Nkurumah hall
 Washiriki toka nchi mbalimbali katika Ukumbi wa Nkurumah......
        endelea kutembelea Konahabari, kwa  maoni / ushauri click kichwa cha post upate maelezo ya kutuma hisia zako....

1 comment: