Sunday, April 15, 2012

MAREHEMU KANUMBA HAKUONEKANA TABATA....!


Siku nne baada ya kifo cha Steven Kanumba, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kuwa marehemu huyo alionekana katika mazingira ya kutatanisha maeneo ya Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam. Taarifa zilieleza kuwa marehemu Kanumba alimtokea muuza duka aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel eneo la Tabata Mawenzi akimtaka amuuzie vocha.
Konahabari ilijaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kupata maoni ya wananchi kuhusiana na kuaminika kwa taarifa hizo.
Kimsingi taarifa hizo haziwezi kuwa za kweli, ni kauli tu za baadhi ya watu kutaka kuleta hisia mbaya kwa marehemu kanumba miongoni mwa wanajamii, alieleza mwanafunzi mmoja wa Kitivo Cha Biashara wa Chuo Kikuu Dar es salaam. Inakuwaje mtu aliyefariki na kuzikwa huku akishuhudiwa na maelfu ya watu aonekane akiwa hai eti anataka Vocha. Vocha ya nini ?  alisisitiza mwanafunzi huyo.
Mwandishi wa konahabari Chuo Kikuu ARDHI alifanya mjadala na baadhi ya wanafunzi kujua mtazamo wao juu ya marehemu Kanumba na taarifa za kuonekana kwake huko Tabata.Kwa ujumla wao walisema kuwa suala hilo si la kweli kwani halina ushahidi wa kutosha na hivyo halina maslahi kwa umma. "Haki ya kuongea inabebwa na ushahidi wa kutosha"
Mtu yeyote anaweza kusema lolote juu ya mtu yeyote wakati wowote, cha msingi ni vyombo vya habari kujifunza maadili ya jamii na kuheshimu utu wa mtu kabla ya kutoa taarifa zake. Walisisitiza wanazuoni hao...


1 comment: