Tuesday, April 10, 2012

MGUNDUZI WA FACEBOOK HUYU HAPA......


Mark Zuckerberg ( kushoto )
  • Ni Myahudi mkazi wa Marekani
  • Kijana mdogo aliyepata mafanikio makubwa na ulimwengu kumtambua kuwa bilionea mwenye mdogo kuliko wote duniani
MTANDAO wa Facebook uligunduliwa na mwanafunzi wa masomo ya sayansi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Mark Zuckerberg, akishirikiana na wanafunzi wenzake, Eduardo Saverin, Dustin Moskovitz na Chris Hughes.

Zuckerberg alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili alipoandika ‘software’ ya mtandao wa Facemash ambao baadae ulikuja kujulikana kwa jina la facebook.

Alitumia maarifa yake ya sayansi ya kompyuta vizuri kwa kuingia katika mtandao wa usalama wa Chuo Kikuu cha Harvard na kunakili picha kutoka kwenye vitambulisho vya wanafunzi wenzake vilivyokuwa vikitumiwa katika mabweni ili kuuboresha mtandao wake wa Facemash.

Mtandao wa Facemash ulianza kufanya kazi Oktoba 28, 2003, na ulifungwa siku chache baadaye na uongozi wa Harvard kuupiga marufuku.

Zuckerberg alifunguliwa mashitaka ya kukiuka masuala ya usalama, kukiuka hakimiliki na kukiuka uhuru wa mtu binafsi, kwa kuiba picha za wanafunzi wenzake alizotumia kuutangaza mtandao wake. Hata hivyo mashitaka yote baadaye yalitupiliwa mbali.

Februari 4, 2004, Zuckerberg alizindua upya mtandao wake na kuupa jina la ‘TheFacebook’.

Siku sita baadaye, Zuckerberg tena aliingia matatani wakati wanafunzi wenzake wa Harvard; Cameron Winklevoss, Tyler Winklevoss na Divya Narendra, walipomtuhumu kuwaibia mawazo yao ya kudhamiria kuanzisha mtandao wa kijamii wenye jina la HarvardConnection, pia kwa kutumia ubunifu wao kutengeneza mtandao wa TheFacebook.

Winklevoss, Winklevoss na Narendra baadaye walimfungulia mashitaka Zuckerberg. Hata hivyo shauri hilo pia lilimalizwa nje ya mahakama.
Uanachama wa mtandao huo awali ulizuiliwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard lakini Zuckerberg aliwaandikisha baadhi ya wanafunzi wenzake ili kusaidia kuukuza mtandao wake: Eduardo Saverin alishughulikia mambo ya biashara, Dustin Moskovitz kama ‘programmer’, Andrew McCollum kama ‘graphic artist’ na Chris Hughes. Kwa pamoja timu hiyo iliupanua mtandao huo hadi katika vyuo vikuu na vyuo vingine vya kawaida.
Mwaka 2004, mwekezaji,  Sean Parker (mwanzilishi wa Napster) alifanywa kuwa rais wa kampuni.
Kampuni ilibadilisha jina kutoka TheFacebook kuwa Facebook,baada ya kununua umiliki wa jina facebook.com mwaka 2005 kwa dola 200,000.
Baadaye Zuckerberg alitambulika kuwa bilionea (mdogo kwa umri) kuliko wote duniani.
hakika, mafanikio hayaangalii umri bali uwezo wa mtu kuzifikilia fulsa na kuzitumia pasipo kujali changamoto ziambatanazo na mafanikio yatarajiwayo. Huu ni ujumbe kwa watu wenye malengo na fikra za ujasiliamali duniani.

2 comments:

  1. dah!,jamaaa ni kichwa!,akili zake zimemwezesha kuwa bilionea.ni jambo kubwa mno.tunapaswa kuiga mfano wake

    ReplyDelete