Friday, April 6, 2012

STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA

 Marehemu Kanumba enzi ya uhai wake

JOHARI- Rafiki mkubwa wa Kanumba na muigizaji wa filamu za Kibongo akilia kwenye msiba wa Kanumba.
 Ndugu jamaa na marafiki wameanza,kukusanyika nyumbani kwa marehemu
toka alfajiri, kwa mujibu wa Shamim Zeze


Steven Kanumba ( muigizaji wa filamu za kibongo ) amefariki dunia usiku kuamkia tarehe saba Mwezi wa nne 2012.
Tukio hilo limetokea nyumbani kwake Sinza, Mwili wake umepelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa filamu na muziki wanazidi kufurika katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili huku wakiomboleza kifo cha marehemu Kanumba.
 konahabari inaendelea kufuatilia zaidi chanzo Cha tukio hili na taratibu za msiba, 

UPDATES: Muigizaji Lulu ambaye ni mpenzi wa Marehemu KANUMBA tayari amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na yupo katika kituo cha polisi cha Osterbay.

Mungu ailaze Roho ya marehemu KANUMBA mahala pema Peponi.....

No comments:

Post a Comment