Monday, April 9, 2012

RAIS MPYA WA MALAWI AMFUKUZA KAZI MKUU WA POLISI


Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi mkuu wa polisi Peter Mukhito,hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali.
Bibi Banda aliapishwa kuwa Rais Jumaamosi baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika wiki iliyopita.
Hakuna sababu iliyotolewa ya kuondolewa kwa Bw Mukhito, lakini vyombo vya habari vimeripot kuwa  mkuu huyo wa polisi anashutumiwa kwa uongozi mbaya wakati wa ghasia za kuipinga serikali zilizotokea mwaka jana.
Mkuu huyo wa polisi alianza kupata sifa mbaya mwaka jana baada ya kumhoji mhadhiri mmoja kwa kulinganisha vuguvugu la upinzani katika nchi za Tunisia na Misri kuwa sawasawa na mgogoro wa mafuta nchini Malawi.
Tukio hilo hatimaye lilisababisha kufungwa kwa tawi moja la chuo kikuu cha nchini Malawi.
Mnamo mwezi wa saba mwaka jana ,yapata watu 19 waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali kuhusu uchumi unaozidi kuzorota nchini humo.

No comments:

Post a Comment